Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba
(NHBRA), Dkt.Simon Kintingu, kuhusu utengenezaji rahisi wa mabati ya
Vigae, wakati Makamu alipofika kuzindua Kambi ya Vijana 400
Wajasiliamali walioanza kambi hiyo leo kwa lengo la kujifunza
utengenezaji wa vigae na ujenzi wa nyumba za bei nafuu, wakati akiwa
katika ziara yake ya Mkoa wa Pwani jana Februari 03,2012.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akifyatua tofali ikiwa ni ishara ya kuzindua raasmi mashine hizo
za kufyatulia matofali ya bei nafuu na uzinduzi wa kambi ya Vijana 400
Wajasiliamali, wakati alipofika kuzindua kambi hiyo iliyopo Kijiji cha
Msoga Mkoa wa Pwani, jana Januari 03, 2012 akiwa katika ziara yake ya
mkoa wa Pwani.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Mohammed Gharib Bilal,
akiangalia na kusikiliza maelezo ya jinsi ya uandaaji wa tofali la bei
nafuu kutoka kwa Fundi Sanifu Ujenzi, Husein Mataka,wakati alipofika
kuzindua kambi ya Vijana 400 wajasiliamali
iliyopo Kijiji cha Msoga Mkoa wa Pwani, Jana Januari 03, 2012 akiwa
katika ziara yake ya mkoa wa Pwani. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)