Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(wa pili kushoto) akiwa katika sherehe za
Maulid ya kuzaliwa Bwana Mtume S.A.W zilizofanyika jana katika viwanja
vya Maisra Suleiman Mjini Zanzibar,(kushoto) Mufti Mkuu wa Zanzibar
Sheikh Saleh Omar Kabbi,(wa kwanza kulia) Jaji Mkuu wa Zanzibar Sheikh
Omar Othman Makungu,na Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji.
(05/02/2012)
Ustadhi Salum Rashid wa Madrsa Qadiria ya Amani akisoma
Maulid Barzanji Mlango wa nne,ambao Waislamu husimama na kumswalia
Bwana Mtume,S.A.W,wakati wa sherehe za Maulid zilizofanyika jana
katika Viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj
Dk.Ali Mohamed Shein,( katikati wakiitikia Dua katika sherehe za
Maulid ya kuzaliwa Bwana Mtume S.A.W zilizofanyika jana katika viwanja
vya Maisra Suleiman Mjini Zanzibar,ikiombwa na Mufti Mkuu wa
Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabbi,(wa pili kushoto)(wa kwanza kulia)
Jaji Mkuu wa Zanzibar Sheikh Omar Othman Makungu,na Kadhi Mkuu wa
Zanzibar Sheikh Khamis Haji,Wazri wa Katiba na Sheria Sheikh Abuu
Bakar Khamis,(kushoto). (05/02/2012)
Mke wa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Pili Balozi
Seif,pamoja na viongozi wengine ni miongoni mwa waliohudhuria katika
sherehe za Maulid ya kuzaliwa kwa Bwana Mtume S.A.W. zilizofanyika
katika viwanja vya maisara Suleiman Mjini Unguja.






No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)