Serikali
imesema imeimarisha ulinzi katika shule ya sekondari ya wavulana ya
Ndanda kufuatia tishio la vurugu linalodaiwa kufanywa na baadhi ya
wanafunzi waliogoma kurudi darasani na kufanya mitihani ya kidato cha
sita.
Katibu
Tawala wa mkoa wa Mtwara Yussuf Matumbo aliiambia Idara ya Habari kuwa
ulinzi umeimarishwa katika shule hiyo ambapo askari wa kulinda usalama
wako wa kutosha ili kuhakikisha kanakuwepo usalama mpaka mitihani hiyo
itakapomalizika.
Kwa
mujibu wa taarifa ya chombo kimoja cha habari iliyoandikwa leo(jana)
ilieleza kuwa juzi Mkuu wa Mkoa huo , Joseph Simbakalia alitoa tamko la
kuwataka wanafunzi waliofukwa
shuleni
hapo kurejea maramoja ili waweze kufanya mitihani hiyo na kuwataka
wafuate sheria na kanuni za shule kipindi chote cha mitihani.
Alisema
kati ya wanafunzi 20 waliokuwa wamegoma kurejea madarasani na kufanya
mitihani hiyo, ni mwanafunzi mmoja tu ndiye aliyeomba radhi na kuendelea
na mitihani.
Aliongeza
kuwa licha ya serikali kuwafutia adhabu ya kuwafukuza shule wanafunzi
hao, wanafunzi 19 wameendelea kugomea mitihani hiyo kwa madai ya
kuishinikiza serikali iwaombe radhi baada ya kutoa taarifa ya
kuwasamehe.
Awali,
wanafunzi hao walifukuzwa shule kutokana na madai ya kutaka kujengwa
kwa msikiti shuleni hapo ili nao waweze kuabudu shuleni kama ilivyo kwa
madhehebu mengine.
Shule
hiyo inamilikiwa na serikali ambapo awali ilikuwa ikimilikiwa na kanisa
la Katoliki, hata hivyo shule hiyo iko katika eneo la kanisa hilo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)