“SAFARI LAGER NYAMA CHOMA 2012” YATANGAZA BAA ZILIZOFANIKIWA KUINGIA FAINALI MBEYA.
Dar es Salaam, Jumatatu Feb 27, 2012:
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo
imetangaza majina ya baa bora zilizochaguliwa kuingia kwenye hatua ya
fainali mkoani mbeya baada ya mchujo wa awali kukamilika kwenye yale
mashindano ya aina yake na ya kuvutia ya kuchoma nyama yajulikanayo kama
“Safari Lager Nyama Choma 2012”
Akizungumza
na waandishi wa Habari kwenye Hotel ya Kebby”s Jijini Dar es Salaam
Jaji mkuu wa mashindano hayo Bwana Douglas Sakibu alisema baa
zilizochaguliwa kuingia hatua ya fainali jijini Mbeya ni.New Cit park,2000 Grocery,Makasini Bar,Savoy Bar na Free Park Bar. ambazo sasa zinasubiri siku ya fainali kwenye uwanja wa CCM Ilomba jumapili ya 04/03/2012
Alisema
baa na majiko hayo yatakutana hapo mapema na kufanya shindano la wazi
ili kuweza kumpata bingwa wa jiji hilo na wananchi watapata nafasi ya
kujionea namna nyama choma inavyoandaliwa katika kiwango cha hali yajuu
kabisa.
Baa
hizi zilizoingia hatua ya fainali zote zina kiwango cha hali ya juu
kabisa na hakika wameonyesha ujuzi na uzoefu mkubwa jambo linaloashiria
kuwepo kwa ushindani mkubwa hivyo ni vyema wakazi wa jiji La Mbeya na
vitongoji vyake wakawahi mapema jumapili pale Ccm Ilomba na kupata wasaa
wa kushuhudia namna nyama zinavyoandaliwa kwa uhodari mkubwa huku
wakiwa na bia yao waipendayo ya Safari Lager.
Kwa
upande wake meneja wa bia ya Safari lager ambao ndio waandaaji wa
Mashindano hayo Bwana Oscar Shelukindo aliwataka wakazi wa jiji la Mbeya
kujitokeza kwa wingi siku ya fainali na pia mashabiki wa baa hizo kuja
kuzishangilia na kuziunga mkono baa zao ili ziweze kuibuka washindi,
sambamba na hayo bado kutakuwa na burudani nyingi toka kwenye bendi
mbalimbali zitakazotumbuiza siku hiyo ili kuweza kutoa burudani kwa
washabiki na wakazi wa jiji hilo kuanzia majira ya saa tano za asubuhi,
pia kutakuwa na zawadi mbalimbali kwa washabiki zitakazotolewa.
Tutaendelea
kuwa karibu na wapenzi wetu wa vinywaji toka Tbl hususani wa bia yetu
ya Safari kwa kuwapatia burudani mbalimbali,Nyama choma bomba zaidi huku
wakipata nafasi ya kujishindia zawadi kibao hivyo ni shindano ambalo
mtu hapaswi kukosa hata kidogo.
Wakati
huo huo majaji wa mashindano hayo leo wanafanya semina na baa
zilizofanikiwa kuchaguliwa jijini Dar Es Salaam kasha kesho kuanza
mchakato rasmi wa kuzitembelea kwenye maeneo yao kwa nyakati tofauti ili
kuweza kupata baa zitakazofanikiwa kuingia hatua ya fainali hivi
karibuni
Semina
ya leo inazishirikisha baa za Huduma bar,Rosehill garden,Kilwa Road
Pub,Pentagon Pub,Texedo Garden,Gadafi Square,Angels Pub,Fyatanga
Bar,Jambo Lee,Hongera Bar,Braek Point Bar,Meeda Bar,Titanic Bar,Mangi
Bar,Africenter Bar,Kisuma bar na Twiga bar .
.Alisema
hii ni fursa ya pekee kwa wachoma nyama na wenye mabaa kuweza kupata
mafunzo yakinifu juu ya uandaaji na uchomaji wa nyama toka kwa wataalam
wenye ujuzi na waliobobea kwenye taaluma hiyo ili kuweza kukuza na
kuboresha biashara zao na hatimae kufikisha kwa wateja kitu kilichokuwa
na ubora wa hali ya juu.
Mashindano
ya Safari Nyama Choma mwaka huu yanafanyika kwa mara ya nne ambapo
mwaka jana washindi wa Jiji la Dar Es Salaam walikuwa Kisuma Bar ya
Temeke Mwembe Yanga,Mbeya walikuwa Mbeya Canival,Kilimanjaro walikuwa
Makanyaga bar ya Soweto na Arusha walikuwa SongaMbele Bar ya Sakina.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)