
Mkuu
wa Kikosi cha Anga 601 KJ Kizuka , Brigedia Jenerali Joseph Kapwani,
ambaye pia ni Base Kamanda wa Vikosi Vilivyopo Ngerengere (aliyeinua
mikono ) akimweleza jambo Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera (
mwenye suti kulia ) wakati Meneja Mradi wa Maji wa Chalinze,Mhandisi
Jeremiah Akonaay , ( kushoto) akisikiliza kwa makini eneo la Ubena
Zomozi , yanapojengwa matenki makubwa ya maji yanayayosukumwa na mitambo
ya umeme kuekelea Vijiji vitano vya Tarafa ya Ngerengere na kambi tatu
za Jeshi,kupitia Mradi wa Maji wa Chalinze.

Meneja
Mradi wa Maji wa Chalinze, Mhandisi Jeremiah Akonaay , (kushoto) akitoa
ufafanuzi wa kitaalamu wa ujenzi wa matenki ya maji yatakayotumika
kusukumwa na mashine kusambaza maji katika Vijiji vitano vya Ngerengere
zikiwemo na Kambi tatu za Jeshi mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel
Bendera ( wapili kulia mwenye suti) juzi ( wa kwanza kulia) ni Mkuu wa
Kikosi cha Anga 601 KJ Kizuka, Brigedia Jenerali Joseph Kapwani, ambaye
pia ni Base Kamanda wa Vikosi Vilivyopo Ngerengere.

Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera ( wa pili kushoto) akisalimiana na
Ofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ) , Luteni Mwajuma
Mwakipesile wa Kambi ya 515 KJ akiongozwa na Kaimu Mkuu wa Kikosi hicho,
Meja Julius Makena, wakati alipotembelea kuangalia utekelezaji wa
miradi ya maji kupitia awamu ya pili ya mradi wa maji Chalinze.


Baadhi
ya mafundi wakiunganisha ndondo katika ujenzi wa tanki kubwa
la kuhifadhi maji kwa ajili ya matumizi ya Askari wa JWTZ Kambi
ya Kikosi cha Anga Kizuka na familia zao katika Tarafa ya
Ngerengere,Wilayani Morogoro, kupitia mradi wa Maji wa Chalinze.Source: HAKI NGOWI





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)