Katibu wa Chama cha Mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola kanda
ya Afrika (CPA Africa) Dk. Thomas Kashililah ambaye pia ni katibu wa
Bunge la Tanzania akifafanua jambo kwa Spika wa Bunge la Afrika Kusini
Mhe. Mninwa Mahalangu (Mb) (Kulia) ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya
Utendaji CPA Afrika wakati wa kikao cha kamati ya Uongozi ya chama hicho iliyokutana Mjini Arusha, leo.
Naibu
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akijadili jambo na Spika wa Bunge la
Afrika Kusini Mhe. Mninwa Mahalangu (Mb) ambaye pia ni Mwenyekiti wa
kamati ya Utendaji CPA Afrika alipofika nchini kuhudhuria Mkutano wa
siku moja wa Kamati ya Uongozi ya Chama cha Mabunge ya nchi wanachama wa
Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika (CPA Africa) unaofanyika mjini Arusha tarehe 25 Februari, 2012
Wajumbe wa sekretariati ya Chama cha Mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola kanda
ya Afrika (CPA Africa), wakiwa katika kikao cha kamati ya utendaji ya
chama hicho kilichofanyika mjini Arusha februari, 25, 2012. Kutoka kulia
ni Dk. Thomas Kashililah, Katibu wa Kanda wa chama hicho ambae pia ni
katibu wa Bunge la Tanzania, Demetrius Mgalami, Naibu katibu wa CPA
Afrika na Said Yakubu Mjumbe wa Sekretariat ya CPA Afrika.
Spika
wa Bunge la Afrika Kusini Mhe. Mninwa Mahalangu (Mb) ambaye pia ni
Mwenyekiti wa kamati ya Utendaji CPA Afrika akiongoza kikao cha kamati
tendaji ya chama hicho walipokutana mjini Arusha jumamosi tarehe 25
Februari, 2012. Kulia kwake ni Spika wa Bunge la Rwanda Mhe. Rose
Mukantabana (Mb) ambaye pia ni Rais wa Chama hicho kwa kanda ya Afrika,
kushoto kwake ni Dk. Thomas Kashililah, Katibu wa Kanda wa chama hicho
ambae pia ni katibu wa Bunge la Tanzania. Picha na Owen Mwandumbya
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)