MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL MGENI RASMI MKESHA WA SHEREHE ZA MAULID MNAZI MMOJA DAR - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL MGENI RASMI MKESHA WA SHEREHE ZA MAULID MNAZI MMOJA DAR

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal(katikati) Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowasa, wakiwa katika sherehe za mkesha wa Maulid, zilizofanyika usiku wa kuamkia leo, jana usiku, katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya kinamama waliojitokeza kuhudhuria sherehe hizo jana.
 Muumin wa dini ya kiislam kutoka Msikiti wa Suni Hanafi wa jijini Dar es Salaam, Muzamil Chaki, akiimba Qaswaida jukwaani kutoa burudani wakati wa mkesha wa sherehe za Mauilid zilizofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini jana usiku.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Muumin wa dini ya kiislam kutoka Msikiti wa Suni Hanafi wa jijini Dar es Salaam, Muzamil Chaki, baada ya muumini huyo kumaliza kutoa burudani ya Qaswaida jukwaani, wakati wa mkesha wa sherehe za Mauilid zilizofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini jana usiku

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages