MAKAMU WA RAIS DKT BILAL ATEMBELEA NA KUWEKA JIWE LA MSINGI SHAMBA LA KUKU MKIU - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL ATEMBELEA NA KUWEKA JIWE LA MSINGI SHAMBA LA KUKU MKIU

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka Jiwe la Msingi katika Kituo cha Mradi wa shamba la Kuku lililopo Kijiji cha Mkiu, Wilaya ya Mkuranga, mkoa wa Pwani, linalomilikiwa na Mtanzania mzawa, Abdulwahd Mohamed (kulia), wakatia akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Pwani leo Januari 02, 2012.
Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa mtaalum, kuhusu ufugaji wa Kuku wa mayai, wakati alipotembelea na kuweka Jiwe la msingi katika kituo cha Shamba la Kuku kilichopo Kijiji cha Mkiu Wilaya ya Mkuranga, Mkoa wa Pwani, leo Januari 02, 2012, wakati akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Pwani.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea na kukagua mabanda ya kufugia kuku katika kituo hicho cha Shamba la Kuku kilichopo Kijiji cha Mkiu Wilaya ya Mkuranga akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Pwani, leo Januari 02, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akitembelea na kukagua mabanda ya kuku katika kituo cha Shamba la Kuku kilichopo Kijiji cha Mkiu Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani, wakati akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Pwani leo Januari 02, 2012. Kushoto ni Mkurugenzi wa kituo hicho, Abdulwahd Mohamed na (kulia) ni Mama Zakhia Bilal.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti wa kumbukumbu nje ya Kituo cha Shamba la Kuku cha Kijiji cha Mkiu, baada ya kuweka jiwe la msingi na kukagua kituo hicho kilichopo Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani, wakati akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Pwani leo, Januari 02, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages