Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akipata maelezo
kutoka kwa sheha wa shehia ya Malindi Bw. Himid Omar, wakati Maalim Seif
alipotembelea eneo la Malindi mjini Zanzibar kuangalia shughuli
zinazofanywa na vijana wa polisi jamii katika eneo la mji mkongwe.Picha
na Salmin Said-0fisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
--
Na Hassan Hamad
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amewataka wafanyabiashara katika eneo la mji mkongwe kushiriki katika shughuli za ulinzi shirikishi kwa kusaidia kuviwezesha vikundi hivyo ili vifanye kazi zake kwa urahisi.

Amesema wafanyabiashara ni wadau muhimu katika kufanikisha shughuli hizo, ikizingatiwa kuwa lengo la polisi jamii ni kuimarisha usalama wa wananchi na mali zao.
Maalim Seif ameeleza hayo huko Malindi mjini Zanzibar baada ya kutembelea sehemu mbali mbali za shehia hiyo kuangalia maendeleo ya kazi zinazofanywa na polisi jamii katika eneo la mji mkongwe.
Amesema
mafanikio makubwa yamepatikana tangu kuanzishwa kwa vikundi vya ulinzi
shirikishi ikiwa ni pamoja na kupambana na vitendo vya uhalimu na
uhifadhi wa mazingira.
Amesema eneo hilo lilikuwa moja kati ya maeneo yaliyokithiri kwa uhalifu na uchafuzi wa mazingira, lakini sasa hali imekuwa ya kuridhisha na kuwataka polisi jamii wa eneo hilo kuongeza juhudi katika kufikia malengo ya kupambana na uhalifu ukiwemo wa matumizi ya dawa za kulevya.
“Mumekataa vitendo viovu katika eneo lenu na mumefanikiwa kwa sababu mumeamua kupambana navyo kwa nguvu zote, hongereni sana kwa kazi nzuri” alipongeza Maalim Seif.
Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa kikundi cha polisi jamii katika eneo la mji mkongwe Bw. Said Mkweche, amesema licha ya kufanya kazi katika mazingira magumu, wamepata mafanikio ambayo ni ya kupigiwa mfano kwa shehia nyengine.
Amesema mafanikio hayo yamepatikana kutokana na kuondoa muhali miongoni mwa wanajamii, na kuzitaka shehia nyingine kuiga mfano huo kwa lengo la kudhibiti vitendo vya uhalifu katika maeneo yao.

Nae Sheha wa Shehia ya Malindi Bw. Himid Omar ameiomba serikali kuunga mkono kwa nguvu zote juhudi zao hizo na kuomba kupatiwa msaada kwa ajili ya matengezo ya banda lao wanalotumia kwa ajili ya kuratibu shughuli za ulinzi shirikishi katika eneo hilo.Wakati huo huo, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Rais amekutana na Balozi wa Pakistan nchini Tanzania na kuelezea haja ya kuendeleza ushirikiano katika nyanja mbali mbali zikiwemo elimu, biashara na utafiti wa kilimo.
Amesema Zanzibar inafuarahia uhusiano mzuri wa muda mrefu uliopo kati yake na Pakistan na kutaka uhusiano huo uendelezwe kwa maslahi ya pande hizo mbili.Amefahamisha kuwa Pakistan ni miongoni mwa nchi zilizopiga hatua katika masuala ya ulinzi ya usalama pamoja na utafiti wa kilimo, na kumtaka balozi huyo kuangalia uwezekano kwa nchi yake kuongeza nafasi za masomo kwa Zanzibar katika fani hizo ili nayo iweze kupiga hatua za maendeleo.
“Kwa sasa tutajifunza kutoka kwenu kutokana na uzoefu mlionao katika nyanja hizo, na si vibaya ikiwa tutapata fursa zaidi kwa vijana wetu kwenda kujifunza nchini Pakistan”, alifafanua Maalim Seif.
Aidha amesema Zanzibar inaweza kushirikiana na Pakistan katika kilimo cha umwagiliaji kutokana na nchi hiyo kuwa na uzowefu mkubwa katika kilimo cha mpunga ambacho ndio zao kuu la chakula kwa Zanzibar.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)