Waziri wa Viwanda na Biashara, Cyril Chami, akihutubia wakati wa hafla hiyo
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo (kulia), akifunua pazia kuonesha
jiwe la msingi wakati wa uzinduzi wa mtambo wa nne wa usafishaji maji
yaliyotumika kiwandani kuwa maji salama kwa matumizi ya binadamu katika
hafla iliyofanyika katika Kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) cha
Arusha, mwishoni mwa wiki.Anayeshuhudia uzinduzi wa mtambo huo
uliogharimu sh. bilioni 3.6, ni Mkurugenzi Mtendaji wa TBL, Robin
Goetzsche.
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo (kulia), akisalimiana na viongozi wa
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), alipowasili katika hafla ya uzinduzi wa
mtambo wa nne wa usafishaji maji yaliyotumika kiwandani kuwa maji salama
kwa matumizi ya binadamu katika Kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania
(TBL) cha Arusha, mwishoni mwa wiki.Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa
Ufundi wa TBL, Gavin van Wijk, Meneja wa Kiwanda TBL Arusha,Bert
Grobbelaar na Mkurugenzi Mtendaji wa TBL, Robin Goetzsche. Wa pili
kulia ni Waziri wa viwanda na Biashara ,Dk.Cyril Chami.
Msimamizi
wa Mtambo Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) wa kusafisha maji taka kuwa
salama kwa matumizi ya binadamu, Said Lwambo kutoka Kampuni ya Talbot
& Talbot, akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo
(wa pili kushoto) na Waziri wa Viwanda na Biashara, Cyril Chami (wa tatu
kushoto) kuhusu usalama wa maji hayo wakati wa uzinduzi wa mtambo huo
uliogharimu sh. bil 3.6 ambao ulifanyika hivi karibuni katika kiwanda
cha TBL Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo (kushoto), akifurahia jambo walipokuwa wakitembelea mtambo huo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)