Mwenyekiti
wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima y Afya Deogratius Ntunkamazina
akisisitiza umuhimu wa kuutumia Mfuko huo kwa manufaa ya Watanzania wote
kwenye Mkutano wa wadau mkoani Lindi.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo Emanuel Humba akieleza mambo mbalimbali ya Mfuko huo kwa wadau wake.
Mwenyekiti wa NHIF, Ntunkamazina akimkabidhi kadi ya CHF mmoja wa waendesha pikipiki ambao wamejiunga na Mfuko huo.
Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Emanuel Humba akipokea maelezo kwa viongozi wa hospitali ya Mkoa wa Lindi ya Sokoine.
wenyekiti
na Mkurugenzi Mkuu wakiangalia moja ya mashuka waliyoyakabidhi
hospitali ya Sokoine, jumla ya mashuka 220 yalikabidhiwa
Wadau wakifuatlia maenelezo ya Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF
Kikundi cha waendesha pikipiki wakiwa wamesimama wakisubiri kupokea kadi zao za matibabu.
--
Na Mwandishi Wetu, Lindi
MWENYEKITI
wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Bw. Deogratius Ntunkamazina
amewataka watoa huduma za afya nchini kuutumia Mfuko huo kwa uzalendo
ili uweze kunufaisha Watanzania wote.
Amesema
kuwa endapo Mfuko huo watautumia kwa ulafi na kwa kughubikwa na
udanganyifu utafilisika na kushindwa kufikia malengo yanayokusudiwa na
Serikali ya kuhakikisha asilimia kubwa ya wananchi wanakuwa kwenye
utaratibu wa Bima ya Afya.
Bw.
Ntunkamazina aliyasema hayo jana wakati akitoa salaam za Bodi ya Mfuko
huo kwenye Mkutano wa Wadau uliofanyika mkoani Lindi uliokutanisha wadau
mbalimbali wakiwemo wakitoa huduma, wanachama, viongozi wa kiserikali,
kidini na wadau wengine.
"Mfuko
wa Taifa wa Bima ya Afya ni fursa nzuri ya kuboresha huduma za afya
nchini hivyo tumieni fursa hii kwa uzalendo mkubwa sana ili baadae
wananchi wote waweze kunufaika na Mfuko huu. Mkiwa walafi na kuweka
udanganyifu mwingi katika kuandaa madai yenu mtaufilisi Mfuko huu,"
alisema Ntunkamazina.
Mwenyekiti
huyo wa Bodi alitumia maneno ya Kiongozi shupavu na mwana Falsafa
Mahtma Gandhi kiongozi wa India, ambaye alinukuu maneno yake aliyowahi
kusema kuwa “Dunia hii ina raslimali za kutosha mahitaji muhimu ya kila
mtu lakini haina raslimali za kutosha ulafi wa kila mtu” mwisho wa
kunukuu. Hivyo kwa kauli hiyo alisisitiza uzalendo katika kuutumia Mfuko
huo.Alisema kuwa endapo Mfuko huo utatumika ipasavyo Watanzania wote
watanufaika lakini ukitumika isivyo utafilisika.
"Jamani
hata Rais wetu ana ndoto kubwa na angependa kabisa aondokapo madarakani
mwaka 2015 aache Watanzania asilimia 50 wakiwa chini ya utaratibu wa
Bima ya Afya hivyo tumuungeni mkono kwa kila mdau kutimiza wajibu wake,"
alisema.
Naye
Kaimu Mkoa wa Lindi ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Magalula Said
naye aliwasisitiza viongozi wote wa Halmashauri kuhakikisha wanaongeza
juhudi katika uhamasishaji wa wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya wa
Jamii.
"Nimejaribu
kupitia takwimu za hapa Lindi na nimegundua kuwa tunazidi kuporomoka
katika suala hili la CHF hivyo kila mmoja kwa nafasi yake ajipange
kuhakikisha hali hii inaondoka na wananchi wetu wanajiunga na Bima kwani
ndio mkombozi wa afya kwa wote hivyo ni lazima tuiweke kama agenda ya
kudumu katika vikao vyetu,' alisema.
Naye
Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Emanuel Humba aliwaomba viongozi wa kisiasa
wakiwemo madiwani kuhakikisha wanasimamia vyema fedha zitokanazo na
mifuko hiyo ili ziweze kutumika katika matumizi sahihi hasa ya dawa.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)