Mtayarishaji wa kipindi cha Ongea na Janet TV talk show pichani kulia akiwa na mmoja wa wadau akifanya nae mahojiano kwenye moja ya kipindi chake.
Ongea
na Janet ni Talk show ambayo inazungumzia mambo yanayotugusa katika
maisha yetu ya kila siku,Inahusisha Jinsia zote na rika zote. Kipindi
changu nilikitengeneza mwaka 2009 june 26 lakini bahati mbaya ilikuwa ni
ngumu sana kupata airtime hasa ikizingatiwa ni kipindi toka nje ya
kampuni husika,bado wahusika hawajakubali kubadilika ila hii "ishu"
digital itasaidia sana. -Sijaajiriwa na Clouds Tv bali tumeingia Mkataba
kama partiners .
Ni
kipindi ambacho sitegemei kishuke bali kitakuwa kinapanda na watu
wategemee mabadiliko,nimeanzia chini napanda juu katika kuleta
changamoto,Natamani watu wenye talents wazitumie bila kuogopa na
wasikate tamaa,kwa mfano,nimehangaika na kipindi changu kwa miaka mitatu
na sasa ndio naanza kuona matunda ya uvumilivu,ubishi wa kutimiza ndoto
na kutokukubali kushindwa kufikia malengo.
Wasijali
maneno ya watu ya kukatisha tamaa,mtu asimame kwenye anachokiamini na
akifanyie kazi haijalishi itachukua muda gani.Nategemea,kuelimisha, kushauri na kuburudisha.
Niliacha
kazi ITV 2008,then nika-join NGO from Canada lakini damu yangu iko
kwenye media...nimeamua kurudi na kuacha kila kitu nyuma. Nataka
kukamilisha ndoto zangu zote zilizosimama kwa miaka 4.
-Kipindi kinaanza tarehe 8 March,alhamis saa 3 kamili
Asanteni sana Wadau.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)