Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwa wamesimama mara baada ya Naibu
Spika wa Bunge Job Ndugay Kuahirisha kikao cha Bunge leo mjini
Dodoma.Pamoja na mambo mengine yaliyojitokeza wakati wa kuahirisha kikao
hicho ni hoja ya Mgomo wa madaktari ambayo iliibuliwa na mbunge wa
Kigoma mjini Peter Selukamba ambaye aliitaka serikali kutoa tamko la
hatma ya mgomo huo ambapo Naibu spika Job Ndugay aliwataka wabunge kuwa
na subira ili Ofisi ya spika ikutane na kamati ya uongozi ya bunge ili
kutoa maamuzi hapo kesho kabla ya kuahirisha mkutano huo wa sita.
Aliyekuwa
waziri mkuu na mbunge wa Monduli Edward Lowasa (kushoto) akijadili
jambo na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu Stephen
Wasira (katikati) na mbunge wa viti maalum CHADEMA Leticia Nyerere leo mjini Dodoma.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa (Kulia)
akizungumza na Zainabu Kawawa mbunge wa viti maalum CCM mara baada ya
kumalizika kwa kikao cha saba cha bunge leo mjini Dodoma.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)