.
Baadhi
ya akina mama walioathiriwa na ajali ya moto katika soko la SIDO jijini
Mbeya, wakiwa wamenyanyua juu hundi ya shilingi milioni 13,350,000/=,
muda mfupi baada ya kukabidhiwa hundi hiyo na mkuu wa Wilaya ya Mbeya
Mhe. Evance Balama (wa tatu kutoka kushoto), muda mfupi baada ya Mkuu wa
Wilaya kupokea hundi hiyo toka kwa meneja wa Exim Bank, tawi la Mbeya
Bw. Geoffrey Kitundu(wa kwanza kushoto)
Meneja
wa Benki ya Exim, tawi la Mbeya Bw. Geoffrey Kitundu (kushoto),
akimkabidhi mkuu wa wilaya ya Mbeya Mhe. Evance Balama, (kulia) hundi ya
shilingi milioni 13,350,000/= fedha ambazo zimetolewa na benki hiyo
kama mkono wa pole kwa akina mama wafanyabiashara katika soko la SIDO,
la jijini Mbeya ambalo liliungua na kuteketea mwishoni mwa mwaka jana.
Katikati ni Makamu Mwenyekiti wa soko hilo, Bw. Wilson Mwakisilwa.
Na mwandishi wetu
HATIMAYE
Benki ya Exim tawi la Mbeya imetimiza ahadi ya kuwapatia wanawake
wafanyabiashara 267 walioathiriwa na moto uliyounguza bidhaa zao katika
soko la SIDO kwa kitita cha shilingi milioni 13.3 ili kuendeleza
biashara zao kwa matumaini zaidi.
Meneja
wa tawi la benki hiyo Geoffrey Kitundu wakati wa hafla fupi ya
kukabidhi msada huo alisema benki yake ilipokea kwa mshituko taarifa za
kuungua kwa Soko hilo na kulazimika kufikiria jinsi ya kuwasaidia
wanawake walioathirika.
“Tulipokea
taarifa za kuungua kwa Soko la Sido kwa masikitiko makubwa. Leo
tunatimiza ahadi tuliyoitoa kwa waathirika na nimatumaini yetu kuwa
itasaidia kuwasogeza mbele kidogo waathirika wa janga la moto pamoja na
familia zao,” alisema Kitundu.
Kitundu alisema benki yake inampango maalum wa kumkomboa mwanamke kwa kutambua mchango wake mkubwa wakuinua uchumi wa taifa.
Nae
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Evans Balama katika hafla hiyo aliushukuru
uongozi wa benki hiyo kwa kutimiza ahadi ya kusaidia ahadi
wafanyabiashara hao na kuzitaka taasisi nyingine kuiga mfano huo. “Desemba
mwaka jana nilikuja kutembelea Soko la Sido baada ya kupata taarifa
kuwa limeungua. Katika soko hilo nilikutana na watalaam wa benki ya
Exim ambao waliahidi kusaidia.
“Tunashukuru
benki ya Exim kwa kutimiza ahadi yao leo. Nimatumaini yetu kuwa fedha
hizi zitasaidia kuwasogeza waathirika hatua moja mbele. Nawahasa
wananake kuzitumia fedha hizi vizuri kuendeleza biashara zao na si
vinginevyo,” alisema Balama.
Balama aliwasii mawanawake hao kukopa na kurejesha mikopo yao kwa haraka iwezekanavyo ilikuendeleza biashara zao. “Msiogope
kukopa fedha benki. Bahati nzuri tumeshapata benki ambayo imeonyesha
ushirikiano. Ombi langu kwenu ni kuhakikisha mnatumia mikopo hii kwa
malengo ya kuboresha biashara zenu,” alisema.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)