WAZIRI WA KILIMO CHAKULA NA USHIRIKA PROF.JUMANNE MAGHEMBE AKIJIBU HOJA
ZA WAKULIMA NA WAKUU WA WILAYA NA VIONGOZI WA HALMASHAURI ZA MBOZI,
MBEYA VIJIJINI, ILEJE NA RUNGWE JANA ALIPOSHAMBULIWA NA VIONGOZI
WENZAKE WA SERIKALI WALIOKUWA WAMEGEUZA KIKAO HICHO KUWA CHA KWAO
WAKATI WAKULIMA WA KAHAWA NDIYO WALITAKIWA KUTOA HOJA.
MKUU WA MKOA WA MBEYA ABBAS KANDORO ALITOA PENDEKEZO KWA WAKULIMA HAO ILI KURUHUSU WAINGIE 10 UKUMBINI HUMO.
MKUU WA MKOA WA MBEYA ABBAS KANDORO ALITOA NENO LA BUSARA NA WAZIRI MAGHEMBE ALIINGIA KWENYE UKUMBI KUJIBU KERO YA KAHAWA
MMOJA
WA WAKULIMA AKIWA ANAELEZA JAMBO KWA WAANDISHI WA HABARI WALIOKUWEPO
MBOZI JANA NA KWAMBA WAO WANATAKA KUUZA KAHAWA MBIVU KATIKA SOKO HURIA
ILI KULETA USHINDANI WA BEI KATIKA ZAO HILO LAKINI WANAZUILIWA NA
HALMASHAURI HIYO HUKU IKIRUHUSU BAADHI YA VIKUNDI VYA WALANGUZI KWA
MANUFAA YAO.
KATIKATI ANAYEONESHA MGONGO NI WAZIRI MAGHEMBE ALIPOZUILIWA NA WAKULIMA
WA WILAYA YA MBOZI ASIINGIE UKUMBINI KWA MADAI KUWA WALIOKUWA
WAMEANDALIWA NA HALMASHAURI YAO WALIKUWA NI WAFANYABIASHARA NA WALA SI
WAKULIMA.
KIKAO KIKIENDELEA
WAKULIMA WA WILAYA YA MBOZI WAKIWA WAMEFURIKA NJE YA UKUMBI HUKU KIKAO KIKIENDELEA
---
· Waziri waghembe aambiwa Wizara imemshinda
· Serikali Mbeya yajitenga, yasema isiingiliwe
· Wakurugenzi wajitoa, wawaachia wanasiasa
Habari hii na Pastor
MWENYEKITI
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Mbozi mkoani hapa Aloyce
Mdalavuma ambaye ni muhanga wa kura za maoni za Ubunge katika uchaguzi
Mkuu 2010, amesema kuwa chama chake ni legelege ndiyo maana kimeunda
Serikali legelege
Hayo
aliyasema jana katika kikao cha pamoja kati ya Waziri huyo, Mkuu wa
mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro, wakuu na wakurugenzi wa wilaya za Mbozi,
ileje, Mbeya Vijijini na Rungwe, wafanyabiashara na wakulima wa zao la
Kahawa.
Mdalavuma
alisema kuwa, wakulima wilayani Mbozi wamekosa pembejeo msimu wa mwaka
2010-2011 na Serikali imekaa kimya jambo ambalo linamkumbusha kauli ya
kwamba chama legelege huunda Serikali legelege.
‘’Ndugu
waziri, umekuja hapa tukifikiri kuwa utazungumzia mustakabali wa uuzaji
na ununuzi wa kahawa mbivu na upatikanaji wa pembejeo lakini
tunashangaa hakuna majibu ya namna hiyo na hii nakumbuka kauli isemayo
chama legelege huzaa serikali legelege’’alisema Mdalavuma huku wadau
wakiguna na Prof, Maghembe akishika tama.
Mwenyekiti
wa Halmashauri hiyo ya Mbozi Erick Ambakisye alimtisha Waziri Maghembe
kuwa endapo anguthubutu kutekeleza kanuni za wizara yake zinazoruhusu
kununua kahawa mbivu wilayani humo ambayo wakulima wanaitaka wakati
Halmashauri haihitaji atakuwa tayari kwenda kwa Rais Jakaya Kikwete ili
waziri huyo achunguzwe.
Alisema
kuwa anavyomfahamu Waziri huyo, anaamini kuwa wizara hiyo ya Kilimo
chakula na Ushirika imemshinda na Jimbo lake pia limemshinda ndiyo
maana wananchi wake hawana uchumi imara.
Kwa
upande wao, wakulima zaidi ya 400 waliofika katika ukumbi wa
Halmashauri hiyo ya Mbozi walimzuia Waziri Maghembe kuingia ukumbini
hapo kwa madai kuwa waliokuwa ndani ya ukumbi walikuwa ni
wafanyabiashara ya kahawa na wala si wakulima na ndiyo maana wao kama
wakulima halisi walikataliwa na viongozi wa Halmashauri kuingia
ukumbini.
Baada
ya hali hiyo ya vuta nikuvute huku Afisa usalama wa wilaya hiyo
akijaribu kuwasukuma wakulima hao ili Waziri aingie ndani na kuzungumza
na ‘’wakulima maalum’’ waliokuwa wameandaliwa bila mafanikio huku
asijue kuwa kulikuwa na wakubwa zake katika msafara huo, ndipo Mkuu wa
mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro alitumia busara ya kuwataka wateue
wawakilishi.
Wakulima
wengi walisema kuwa taarifa aliyokuwa amepewa na viongozi wa Mkoa wa
Mbeya iliyosema kuwa uuzaji wa kahawa mbivu inawaingizia hasara siyo ya
kweli bali ililenga kuwanufaisha watu wachache wakiwemo vigogo wa
Halmashauri zinazolima zao la kahawa mkoani Mbeya.
Mkulima
Abrahamu Nzowa alisema kuwa, wakati Serikali na baadhi ya watendaji wa
Halmashauri hizo zikiwa zinaipiga vita biashara hiyo hasa kampuni ya
Lima Ltd inayonunua zao hilo kwa bei kubwa kuliko vikundi ambavyo
viongozi hao wanamanufaa navyo, vikundi vinaendelea kuwanyonya wakulima
hali ambayo wamesema inaleta kutoelewana miongoni mwao.
Aidha
walisema kuwa kwasababu kahawa ni mali yao hawataacha kuuza kahawa hiyo
mbichi kwa kampuni ambayo itakuwa inanunua kwa bei nzuri licha ya
wilaya na mkoa kukataza kuuza kahawa hiyo.
Mkuu
wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro alimweleza Waziri Maghembe kuwa msimamo
wa Serikali ya mkoa wa Mbeya ni kwamba haitaki kusikia uuzaji na
ununuzi wa kahawa mbivu mkoani hapa mpaka pale wakulima
watakapoandikishwa na kutambulika.
‘’Sisi
kama mkoa wa Mbeya tuliazimia katika vikao halali vya wadau wa mkoa na
kwamba hatutaki biashara ya kahawa mbivu na kwasababu hapa hakuna
wakulima walioandikishwa hawa wote si wakulima halali kisheria hivyo
mpaka hapo tutakapokamilisha zoezi la kuwaadikisha ndipo tutakapochukua
maoni yao’’ alisema Kandoro kwa kujichanganya.
Akizungumza
na waandishi wa habari nje ya ukumbi huo baada ya kuogopa hoja za Wakuu
wa wilaya, wenyeviti wa Halmashauri za wilaya hizo Nne huku wakurugenzi
wote wakikataa kuzungumzia suala hilo lililochukuliwa kisiasa zaidi,
Waziri Maghembe alisema kuwa hatengui kanuni zenye baraka za Wizara
bali anachotaka bei ziboreshwe kwa wakulima.
‘’Mimi
sijatengua kanuni za Wizara na Bodi ya kahawa juu ya ununuzi wa kahawa
m,bivu bali nilichokuwa nasema ni kwamba lazima wilaya zisimamie sheria
na kuhakikisha bei kwa wakulima wa kahawa zinasimamiwa na kulipwa vema
lakini Serikali ya mkoa nyie mmeisikia haitaki biashara hiyo’’ alisema
Waziri Maghembe.
Alisema
licha ya hayo yote kila mfanyabiashara wa kahawa ama mnunuzi ni lazima
awe na leseni ya biashara na haruhusiwi kununua kahawa kwa mkulima
ambaye hajaandikishwa ili kudhibiti ukwepeji mapato ya Serikali kupitia
biashara hiyo kama ilivyo sasa wilayani humo.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa bodi ya kahawa nchini Adolph Kumbulu na
mwanasheria wa Wizara ya kilimo walisema kuwa ununuzi wa kahawa mbivu
umeongeza tija ya ubora wa kahawa Tanzania kutokana na ubora wa
usindikaji wake tofauti na usindikaji unaofanywa na wakulima.
Hali
hiyo ya mkanganyiko wa uuzaji na ununuzi wa kahawa mbivu (Cherry)
imeleta utengano wa baadhi ya wakulima ambapo Serikali hasa vyombo vya
usalama vinatakiwa kuliangalia kwa umakini kutokana na hali ilivyo ya
wananchi kujengeana chuki ikiwa ni pamoja na kuijengea chuki Serikali.
Ubora
wa kahawa upo katika ngazi nne ambazo ni P1,P2,P3 na Ponds, ambapo P1
inatoa madaraja Nane ambayo ni AA, A, B, PB, C, AF na F ambapo madaraja
yanayouzwa nje ya nchi ni AA,A,B, PB na daraja C.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)