
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Erwin Telemans, akifafanua jambo
katika mkutano wa kuhitimisha mradi wa kuwawezesha Waelimishaji Rika
wenye Ulemavu kuwa waelimishaji kwa walemavu wenzao juu ya vita dhidi
ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi na Ukimwi, jiji Dar es Salaam.
Kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Jamii wa CCBRT, Brenda Msangi.

Mkurugenzi wa Huduma za Jamii wa CCBRT, Brenda Msangi akizungumza katika mkutano huo.

Mwelimishaji Rika, Neema Abas kutoka Ngamiani Tanga,mwenye ulemavu wa kutosikia, akichangia hoja katika mkutano huo.

Mwelimishaji Rika Farida Chamwana kutoka Kilosa Morogoro, akitumia lugha ya alama kuchangia hoja wakati wa mkutano huo.

Meneja
Mradi wa CCBRT, Clement Ndahani, akijibu maswali mbalimbali
yaliyoelekezwa upanda wao na watu wenye ulemavu waelimishaji rika leo
katika Hoteli ya Serena, Dar es Salaam.

Mwenyekiti
wa Watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi, Vitalis Makayuga akichangia
hoja na kuomba CCBRT isisitishe mpango huo ili walemavu waendelee
kuelimika juu magonjwa hayo.

Hamis Mchuro ambaye ni Muelimishaji Rika kutoka Kijitonyama, akiipongeza CCBRT kwa kuwezesha waelimishaji rika walemavu nchini

Baadhi
ya Watu wenye Ulemavu wakiwa katika mkutano wa kuhitimisha mradi wa
kuwawezesha Watu wenye Ulemavu kuwa waelimishaji kwa walemavu wenzao
juu ya vita dhidi ya maambukiz.Picha na Mdau Richard Mwaikenda





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)