Picha juu ni Mratibu wa Ujenzi wa nyumba za muda za waathirika wa mafuriko, Aidan David Mwalyambwile (kulia)
wa Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania(Tanzania Red Cross), akiwapatia
maelezo vijana wa kikosi cha maafa na uokoaji mkoa wa Dar es Salaam
(Action team) namna ya kujenga nyumba hizo katika viwanja vya Mabwepande jijini Dar es Salaam, mwishoni mwaka wiki, mpaka sasa nyumba zaidi ya 200 zimeshajengwa chini ya Msalaba Mwekundu.
TRC's Action team, wakiwa katika ujenzi wa nyumba hizo za muda katika viwanja vya Mabwepande,Picha na Andrew Chale-Mjumbe wa kikosi cha maafa na uokoaji cha msalaba mwekundu Tanzania
--
Na Andrew Chale
Ujenzi
wa makazi ya muda huko Mabwepande unaendelea kwa takribani wiki ya pili
sasa ambao unafanywa na kikosi maalum cha Maafa na Uokoaji mkoa wa Dar
es Salaam (Action Team) cha Msalaba Mwekundu Tanzania (Tanzania Red
Cross), ambapo muda wowote kuanzia sasa kaya 300 zitapelekwa huko kwa
ajili ya kuanza maisha mapya sambamba na kujenga nyumba zao za kudumu.
Viwanja
hivyo kwa ajiri ya waathirika wa mafuriko jijini Dar es Salaam, vipo
nje ya jiji la Dar Kilometa 6 kutoka njia panda ya Bunju B, mpaka kufika
huko Mabwepande huku usafiri wake mkubwa ukiwa ni pikipiki kwa nauli
ya shilingi 1500/2000, huku kwa taxbubu nauli ikiwa ni bukubuku kwa
abiria wanne.
Mpaka
sasa tayari kikosi hicho maalufu kama 'TRC's Action Team', kimeweza
kufikisha nyumba za muda zaidi ya 200 na tayari Rais Jakaya Kikwete
ameweza kujitembelea na kujionea hali halisi ya utendaji wa kazi wa
kikosi hicho ambacho pia kinashirikiana na jeshi la kujenga Taifa 'JKT'.
Katika
ujenzi huo unaosimamiwa na mtaalamu maalum wa TRC's, Aidan David,
alisema kua nyumba hizo ni imara na zinauwezo mkubwa wa kukaa familia
tano kwa kila moja na zinadumu iwapo mtumiaji ataitumia kwa ukamilifu
mkubwa sambamba na kuifanyia marekebisho kidogo.
Aidan
alisema kua, watahakikisha wanajenga nyumba zaidi ya 300 katika viwanja
hivyo na zitakua faraja kwa wakazi watakaoletwa hapo na watazitumia
huku wakiendelea na ujenzi wa nyumba zao za kudumu.
Uchunguzi
uliofanywa na mwandishi wa habari hizi alibaini kasoro mbalimbali
ikiwemo ufinyu wa upatikanaji huduma muhimu ikiwemo za maduka na vyakula
huku vyakula vilivyopo vikiwa havikidhi mahitaji halisi ya walaji
wanaofika kila kukicha katika maeneo ya viwanja hivyo kwa sasa.
Hivyo
wafanyabiashara wa makampuni ikiwemo ya simu,vinywaji na chakula
wanashahuriwa kufika eneo hilo la viwanja hivyo ilikurahisisha tatizo la
ukosefu wa mahitaji muhimu ambapo kwa siku Mabwepande kwenye mradi huo
wa viwanja inapokea watu zaidi ya 100 mbali ya wafanyakazi wa Msalaba
Mwekundu,askari wa JKT, wataalamu wa barabara na Wakandarasi wanaofanya
savei na kupima viwanja hivyo.
....Onyo
epuka matapeli tayari wameshavamia kwenye viwanja hivyo na namba za
nyumba za watu wa jangwani wakidai kua viwanja hivyo wakipewa watawauzia
watu hivyo uchunguzi umebaini watu wengi wanamiminika huko wakiangalia
mianya ya kufanikisha hadhima hiyo ikiwemo kuwahadaa maafisa ardhi wa
Kinondoni na kamati ya maafa ya waziri mkuu.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)