Katibu
Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza katika kongamano na
mkutano mkuu wa Jumuiya ya Wanawake CUF Wilaya ya Magharibi huko hoteli
ya Bwawani.
Katibu
Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na wanachama wa CUF
wakati akijiandaa kuingia katika kongamano na mkutano mkuu wa Jumuiya ya
Wanawake CUF Wilaya ya Magharibi huko hoteli ya Bwawani.
Vijana wa sarakasi wakitoa burdani katika kongamano la CUF wanawake huko hoteli ya Bwawani
Vijana wa kike wa CUF wakitoa burdani katika kongamano la CUF wanawake huko hoteli ya Bwawani.
---
Wanawake
nchini wamehimizwa kujiandaa na kupigania nafasi za uongozi katika
vyama na serikali, na kuachana na mtazamo wa kupatiwa nafasi hizo kwa
upendeleo.
Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad huko hoteli ya Bwawani alipokuwa akifungua Kongamano na Mkutano mkuuu wa Jumuiya ya wanawake wa chama hicho kwa Wilaya ya Magharibi.
Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad huko hoteli ya Bwawani alipokuwa akifungua Kongamano na Mkutano mkuuu wa Jumuiya ya wanawake wa chama hicho kwa Wilaya ya Magharibi.
Maalim
Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar amesema
wanawake wanao uwezo mkubwa wa kuongoza na kwamba iwapo watapigania na
kupata nafasi hizo wanaweza kufanya vizuri zaidi na kuleta mabadiliko ya
haraka ya maendeleo katika taifa.
Amewataka wanakongamano na wajumbe wa mkutano huo kuwaandaa vijana wa kike katika uongozi kwa kuwapatia elimu bora ili waweze kushika nafasi za uongozi na kulisaidia taifa katika mchakato wake wa maendeleo.
Amewataka wanakongamano na wajumbe wa mkutano huo kuwaandaa vijana wa kike katika uongozi kwa kuwapatia elimu bora ili waweze kushika nafasi za uongozi na kulisaidia taifa katika mchakato wake wa maendeleo.
Amesema wanawake wanaopata fursa za uongozi wamekuwa wakifanya vizuri katika nafasi zao akiwatolea mfano waziri katika ofisi yake Mhe. Fatma Abdulhabib Fereji na Spika wa Bunge Mhe. Anna Makinda. Pia ameitolea mfano nchi ya Rwanda ambayo imekuwa ikipiga hatua za haraka za maendeleo huku wabunge wengi wa nchi hiyo wakiwa wanawake.
Amefahamisha kuwa wanawake wanaweza kutekeleza majukumu makubwa kama walivyo wanaume katika nafasi mbali mbali zikiwemo majaji, mameneja, marubani na wahandisi.
“Ukija katika ngazi wa chini za elimu utaona wanawake ni wengi kuliko wanaume lakini kila ukienda mbele wanawake wanapungua kidogo kidogo, hivyo mnapaswa mjipange na kuwahamasisha ili wasirudi nyuma” alitanabahisha Maalim Seif.
Kuhusu mchakato wa katiba mpya, Maalim Seif ametumia fursa hiyo kuwaasa wanawake kuitumia fursa hiyo kutoa maoni yao kwa lengo la kutetea maslahi ya wanawake kikatiba, sambamba na maslahi ya Zanzibar kwa ujumla.
Amezitaka jumuiya za kinamama kushirikiana na jumuiya za vijana katika chama hicho katika jitihada za kukiimarisha chama kwa kuendeleza umoja na ushikamano, ili kukijengea mazingira mazuri katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
“Uhai wa Jumuiya hizi ndio uhai wa chama, ikiwa wanajumuiya mtashirikiana basi chama chetu kitakuwa imara zaidi na kupata mafanikio makubwa zaidi katika uchaguzi ujao kuliko uchaguzi uliopita wa 2010”, aliasa Maalim Seif.
Akizungumzia uhai wa chama Maalim Seif amesema chama hicho bado kiko imara na kinaendelea na shughuli zake kama kawaida, tofauti na kinavyoelezwa na baadhi ya watu.“CUF bado iko ngangari kinoma”, alidokeza.
Mapema akiwasilisha mada inayohusu nafasi ya mwanamke katika uongozi, bwana Hashul Nassor Ali amesema wanawake wanayo nafasi kubwa ya kushiriki na kufanya vizuri katika uongozi, na kuwataka kupigania nafasi hizo.
Akizungumzia kuhusu maadili ya uongozi mjumbe wa Jumuiya ya Vijana CUF Wilaya ya Mjini Bwana Omar Saleh Sultan amewataka viongozi wa ngazi mbali mbali kulinda maadili ya uongozi na kuachana kabisa na ubinafsi na majungu kwa vile mambo hayo ni miongoni mwa mambo yanayorejesha nyuma maendeleo ya taasisi yoyote.
Pia ametumia fursa hiyo kwa niaba ya wajumbe wa kongamano na mkutano huo kulipongeza baraza kuu la uongozi la chama hicho kwa kuwavua uanachama wanachama wake wanne akiwemo Mbunge wa Jimbo la Wawi Mheshimiwa Hamad Rashid Mohd.
Na
Hassan Hamad
Hassan Hamad
Ofisi Ya Makamu Wa Kwanza Wa Rais Zanzibar
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)