TRIBUTES TO THE LATE MO CHELLA, FREESTYLE KILLER - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

TRIBUTES TO THE LATE MO CHELLA, FREESTYLE KILLER

Hello Wadau,

Kufuatia msiba uliotupata wadau wa HIP HOP Mwanza, kwa kuondokewa na
aliekua Rapper na Free-styler mzuri to the extent alikua mshindi wa Pili katika STR8 MUZIK FREESTYLES COMPETITON 2011, FRANK BUCHELA a.k.a MO CHELLA aliekua aki-represent kundi la "SWAGGA-MAKERS" baadhi ya watu tumefanya Tacks kwa ajili ya kumuenzi sababu tulikua nae pamoja sana katika kuhakikisha HIP HOP inaendelea kua na heshima yake.

Track ya kwanza ni yangu nimemshirikisha Mwana- Swagga-Maker YANOO katika verse ya 3, DR. EDDO toka Zoo Records aliefanya Beat na kuimba Chorus, Wakati T-NOCK ame-harmonise track yote na BARAKA alimpokea kidogo YANOO ktk verse ya 3.

Vocals na mixing ni kazi ya DEE CLASSIC toka YUNG DON RECORDS...

1. The Rocker Feat. Yanoo & Dr. Eddo - G.O.N.E. (RIP MO CHELLA)

2. Rock City All Stars - R.I.P. MOCHELLA (Produced By DEE CLASSIC)



The Rocker - G.O.N.E (R.I.P Mo Chella) Ft. Yanoo, Dr. Eddo, T-Nock & Baraka produced by Dee Classic & Dr. Eddo.mp3



R.I.P MO CHELLA-ALLSTAR FROM ROCK CITY PRODUCED BY DEEY CLASSIC MASTER.mp3
---
SONG: For My Brother (R.I.P. MO CHELLAH)
Written By Ezden The Rocker

VERSE I:


Kilio huanza mfiwa, ndipo wa mbali wanaingia/

Hizi siku zinahesabiwa, huwezi jua tapotimia/
Umeniacha na maneno, kama baridi na urusi/
kinywa jumba la maneno, kamwe nisiongee tusi/
Beef zilotokea, vijambo kwenye mitaa/
Mwanga nakuombea, haya maisha ni vita/
Ulinipa nyingi sana, changamoto kwa Freestyle/
Leo tumetengana, battle zangu haziwezi fika/
Wahenga walishasema, Chanda chema huvikwa pete/
Ma-Mc walikusoma, kwa mistari isio na ubwete/
Kitanda usicholala, huwezi jua kunguni wake/
Machungu ni zaidi ya msala, subiri matokeo yake/
Tulisaka sana heshima, Na hela sio publicity/
Mashairi yenye vina, walipiga salute - Ti!/
Mashavu tulikomba, kwa mashairi tuliwabonda/
Ndugu sa msijekonda, cha msingi tuzidi kuomba/


VERSE II:


This is for my brother, from another mother/

Nauchungu siisomi ladha, lakini nakaza stanza/
Kumbuka mara ya kwanza, mimi nafika mwanza/
Wewe kina P.M.P na Flexx wa Mwanza Kwanza/
Mlinipokea vizuri, A2P Mitaa ya Uhuru/
Vitu vingi tuliendana, hasa hii mitindo huru/
Sina cha kufanya, Mungu tu namshukuru/
Mi na Hip Hop tashikana, kusongesha hili duru/
Kivuli cha fimbo, hakimfichi mtu jua/
Leo naimba wimbo, kesho sijui ntakapokua/
Tuangalie matendo, huenda ndo yatatuokoa/
Umenipiga nembo, moyoni sitoiondoa/
Alichoandika Mungu, lazima kitimilike/
Yes moyoni nina uchungu, Mo Chella peponi ufike/
Utabaki kumbukumbu, Milele usisahaulike/
Documentary ya MLAB ile alotu-shoot Duke/

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages