TAARIFA KWA UMMA
ya HakiElimu Tarehe Jumanne, Januari 17, 2012 saa 8:14 asubuhi
Marafiki wa Elimu Ndugu Jordan Nyembe ( Anayeonekana katika picha hapo juu ) .
HakiElimu
ni asasi isiyo ya kiserikali iliyoanzishwa mwaka 2001 dira yake
ikilenga kufikia usawa, ubora, haki na demokrasia katika utoaji wa elimu
katika jamii, ambapo elimu inakuza usawa, ubunifu, udadisi, na
demokrasia.
Ili kuifikia dira yake, HakiElimu inawasaidia
wananchi kujua haki na wajibu wao kwa kuwapa taarifa mbalimbali ili
waweze kushiriki katika ngazi mbalimbali za maamuzi na kuchangia
kuboresha elimu na demokrasia. Harakati za Marafiki wa Elimu ni
mojawapo ya nyenzo zinazotumika kuhamasisha ushiriki huu wa wananchi.
Hizi ni harakati za wananchi, mashirika na taasisi zenye nia ya kuongeza
kasi ya kuleta mabadiliko chanya katika elimu na demokrasia nchini.
Harakati hizi zilianzishwa mwaka 2003 kama mojawapo ya fursa kwa
wananchi kubadilishana mawazo, uzoefu na hatua za kuleta mabadiliko
katika elimu. Takribani wananchi 35,000 kutoka nchi nzima, vikiwemo
vikundi na asasi mbalimbali, wamejiunga na Harakati hizi mpaka sasa.
Pamoja
na nia nzuri ya HakiElimu kupigania haki ya wananchi kushiriki katika
ngazi mbalimbali za maamuzi na kuichagiza serikali kutoa huduma bora za
jamii hususani elimu; inasikitika kuhusu mwenendo wa Rafiki wa Elimu Ndugu Jordan Nyembe, mwenye kadi ya uanachama namba 320915, kutumia vibaya jina la HakiElimu na Mtandao wa Marafiki wa Elimu kinyume na malengo yake kwa:
- Kujitambulisha kwenye mitandao ya kijamii kama vile Facebook, kuwa yeye ni mwajiriwa mtafiti wa HakiElimu.
- Kuomba wahisani kuchangia shughuli za wanamtandao kwa kutumia jina la HakiElimu
- Kuandika barua/barua pepe kwa watu, wahisani, na balozi mbalimbali akijitambulisha yeye kama mtafiti kutoka asasi ya HakiElimu
Vitendo hivi viko kinyume na misingi inayojenga Harakati za Marafiki wa Elimu
na vinaharibu taswira ya asasi ya HakiElimu kwa wadau mbalimbali.
HakiElimu imejitahidi kuwasiliana na Ndugu Nyembe kwa lengo la
kumwelewesha kuacha kutumia jina la HakiElimu na Harakati za Marafiki wa Elimu bila ya mafanikio. Ili kuzuia upotoshaji zaidi, HakiElimu imeazimia kumfuta katika Harakati za Marafiki wa Elimu Ndugu Jordan Nyembe ( Anayeonekana katika picha hapo juu ) .
Kwa taarifa hii, HakiElimu inawatahadharisha wadau wote, wakiwemo Marafiki wa Elimu, kujiepusha na vitendo vya kitapeli na ulaghai wowote vinavyofanywa na ndugu huyu kwa kutumia ama jina la mtandao wa Marafiki wa Elimu
au HakiElimu. Matumizi ya mtandao huu yanasimamiwa na misingi na
malengo yake kama ilivyofafanuliwa kwenye kitabu cha mwongozo wa Marafiki wa Elimu.
Kwa
ufafanuzi zaidi, wasiliana na Ndugu Pius Makomelelo wa Idara ya
Ushiriki wa Jamii kwa barua pepe rafiki@hakielimu.org au S.L.P 79401,
Dar es Salaam.
Elizabeth Missokia
Mkurugenzi Mtendaji
HakiElimu
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)