TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
NDUGU WANAHABARI
Awali
ya yote hatuna budi kumshukuru Mwenyezi Mungu mola wa viumbewote. Pili
tuna kushukuruni kwa kuitikia wito wetu licha ya kuwa namajukumu mengi
ya kutoa taarifa kwa wananchi.Kwa mara ya kwanza
tumeamua
kukutana nanyi. Nasi tunatoa taarifa yetu hii kwenu ilimuifikishe kwa
Watanzania na wapenda amani wote duniani. Tunakuusienijuu ya ukweli na
uaminifu katika kuripoti taarifa hii.Tuna kuusieni tena
kuripoti taarifa hii bila ya kupotosha maana iliyokusudiwa.Kutakuwa na
nafasi ya maswali ili kuuliza ikiwa kunasehemu ambayohaikueleweka.
NDUGU WANAHABARI
Tuliowaita
ni viongozi wa Jumuiya ya Wanafunzi na Vijana wa KiislamuTanzania yaani
Tanzania Muslim Students & Youth Association (TAMSYA).Jumuiya yetu
inatambulika kisheria na inafanya kazi zake kwa kufuatasheria za nchi.
NDUGU WANAHABARI
Jumuiya
yetu kama inavyojieleza inashughulika na malezi ya wanafunziwafuasi wa
dini ya kiislamu waliopo katika shule, vyuo vya kati navyuo vikuu na
vijana wa kiislamu kwa ujumla. Jumuiya hii inawalingania waishi kwa mujibu wa mafundisho ya dini ya Uislamu.
NDUGU WANAHABARI
Tumeamua
kukutana nanyi ili kuzungumzia mambo ambayo yanawapatawanafunzi
waislamu waliopo kwenye shule na vyuo vya serikali kwa mudamrefu.
Wanafunzi waislamu wamekuwa wakinyanyaswa na kuwekewa vipingamizi vya makusudi ambavyo vinasababisha kufanya vibaya katikamasomo yao pindi wakiwapo shuleni.
NDUGU WANAHABARI
Sheria
ya nchi inaruhusu uhuru wa kuabudu na kuchagua dini. Kwa mujibuwa dini
yetu ya uislamu ibada haimaliziki kwa kuingia msikitini nakuswali tu
bali Uislamu wenyewe ni mfumo kamili wa maisha. Ibada nikila jambo
analolifanya muislamu na linaloridhiwa na Mwenyezi Mungulikiwa katika
muundo wa vitendo au kauli za dhahiri na kificho.
NDUGU WANAHABARI
Tumepata malalamiko kutoka kwa wanafunzi waislamu wakikatazwa kuvaa HIJABU shuleni, Tumepata
mashitaka kutoka kwa wanafunzi waislamu wakinyimwa sehemu
zakusalia/kufanya ibada ya sala katika mazingira ya shule na
vyuo.Tumepata mashitaka juu ya kupangwa makusudi matukio mbali mbali ya shule
katika nyakati za sala za waislamu. Mfano sherehe za Mahafalizinapangwa
kufanyika siku za Ijumaa muda wa sala, Ratiba za mitihanivyuo vikuu
hazizingatii muda wa swala ya Ijumaa .kurefusha muda wa kusimama
mstarini (Parade) mpaka muda wa swala unapita.Wanafunzi waislamu
wamekuwa wakikatazwa kuvaa kofia au kanzu baada yamuda wa masomo katika
shule za bweni huku wakristo wakiwa wanashinda na Rozari masaa 24.Waalimu wanaofundisha somo la maarifa ya uislamu wanawekewa vikwazo mbalimbali wakati wachungaji wanapishana katika shule bila vikwazo kwenda kufundisha baibal knowledge. Vipindi
vya dini vinawekwa katika ratiba za shule muda wa saa saba mchana siku
ya ijumaa wakati ambao wanafunzi wa kiislam wanapaswa kuenda msikitini
kwa ajili ya swala ijumaa.
NDUGU WANAHABARI
Tutatoa
mifano kadhaa katika maeneo tofauti ambayo wanafunzi waislamwamefanyiwa
madhila, manyanyaso na udhalilishwaji ikiwa ni pamoja na kutukaniwa
Mungu wao,mtume wao na kitabu chao (Quran tukufu) na TAMSYA imefuatilia
bila ya mafanikio.
SHULE YA SEKONDARI KIZUNGUZI WILAYANI KILOSA –MOROGORO
Mwanafunzi
wa kidato cha nne, Frank Thobias Cosmas, aliandika waraka ulioukashifu
uislamu, Qurani tukufu na Mtume Muhammad Sallalahu alaihi
wasallam.Wakati wanafunzi wakristo wakiwa wanaubandika katika mbao za
matangazo shuleni hapo na kusambaziana waraka huo Tarehe 13/05/2011
mwanafunzi muislamu Saidi Suleiman aliupata na kuufikisha kwa viongozi
wa wanafunzi waislamu na hatimaye malalamiko hayo yalifika kwa mkuu wa
shule.Mkuu wa shule alimpa Adhabu Yule mwanafunzi aliye peleka taarifa
na viongozi
wa wanafunzi waislamu walisimamaishwa shule kwa muda wa siku 21, na
Yule aliyendika waraka huo alibakishwa kufanya kazi za shule.Tukio hili
liliripotiwa kwa Mkuu wa polisi Morogoro, Afisa Elimu
Mkoa
Morogoro na ofisi ya mkuu wa wilaya ambao walipuuza. Hatua hiyo
ilisababisha waislamu wa Mkoa wa Morogoro kuandamana kwa amani siku ya
Ijumaa tarehe 5 Agosti, 2011.
PIA SHULE YA SEKONDARI ULONGONI – DAR ES SALAAM
Siku
ya Alhamisi,tarehe 27/01/2011Mkuu wa shule hiyo aliwalazimisha
wanafunzi wa kike wa shule hiyo kuvua Hijabu wakati wa zoezi la kupiga
picha kwa ajili ya Mtihani wa kidato cha nne.Alifanya hivyo kwa chuki za
udini kwa sababu waraka wa baraza la mitihani unaotoa maelekezo ya
namna na utaratibu wa kupiga picha kila mkuu wa shule amepatiwa na
haukuagiza hivyo.
SHULE YA SEKONDARI ENGUSERO KIBAYA –KITETO
Mkuu
wa shule hiyo kwa kushirikiana na Kaimu katibu Mkuu wa mkoa wa Manyara
kwa barua yake ya Kumb.Na.FA.58/347/01/27 aliwaamrisha wanafunzi wavunje
msikiti uliopo hapo shuleni kwa madai ya kwamba katika shule za
serikali hairuhusiwi kujengwa nyumba ya ibaada. Lakini sikweli kwa kuwa
zipo shule nyingi za serikali zilizo na nyumba za ibada makanisa tena
makubwa sana. Mfano Shule ya sekondari Ndanda, Shule
ya sekondari Umbwe, Lyamungo Sekondari, Pugu Sekondari Dar es salam na
karibu shule zote kubwa za Serikali nchini. Huu ndio udini na mfumo
kristo unaolalamikiwa na unaoliyumbisha taifa.
SHULE YA SEKONDARI ALDERSGATE BABATI MANYARA
Mkuu
wa shule hiyo aliwanyima wanafunzi waislamu darasa kwa ajili ya kusomea
somo la maarifa ya uislamu na kuwaambia kama wanataka kusoma somo la
dini wachanganyike na wakristo ambao wamepewa chumba cha kusomea shuleni
hapo, Jambo ambalo ni kinyume na sheria na kanuni za nchi.aidha alipiga
marufuku uvaaji wa hijabu shuleni hapo kwa taarifa tuliyo letewa ya
17/03/2011.
SHULE YA SEKONDARI LUGOBA
Mwalimu
aliwataka wanafunzi waislamu washerehekee Krismas walipokataa
akawaambia tutaweka Taarabu maana waislamu mnapenda sana taarabu.Siku ya
21/01/2011 kwa makusudi Makamu Mkuu wa shule hiyo aliingia na viatu
katika eneo la chumba wanachotumia waislamu kuswalia na kuwaamuru watoke
katika chumba hicho wakati wa swala.Makamu Mkuu huyo alikwenda tena
siku ya tarehe 31/01/2011 kwa hasira na
kundi kubwa lililo sheheni wanfunzi wakristo kwa ajili ya kuwafanyia
fujo waislamu waliokuwa wakiswali. jambo ambalo lileta tafrani kubwa
shuleni hapo cha kusikitisha ni kuwa ukweli ulipotoshwa
na hatimaye wanafunzi waislamu walionekana ndio chanzo cha tatizo.
SHULE YA SEKONDARI ILBORU ARUSHA
Mwanafunzi Juma Hassan alifukuzwa shule 13/01/ 2006 ikiwa ni wiki tatu kabla ya kuanza kwa mitihani ya kidato cha sita. Sababu ya kufukuzwa shule ilidaiwa alimsukuma Mama Mkwizu mwalimu sheleni hapo alipotaka kuingia msikitini.
SHULE YA UFUNDI TANGA JIJINI TANGA
Mwaka
2006 Mkuu wa shule hiyo bwana T. Z. Kinala amekuwa na tabia ya Kutoa
salamu ya HALELUYAH mstarini wakati wa PAREDI huku akijua kwamba
wanafunzi walio mbele yake ni mchanganyiko wa waislamu,wakristo na watu
wa dini nyingine.Lakini si hivyo tu, Tarehe 24/7/2006 mkuu wa shule
alileta kikundi cha kwaya cha kanisa wakati PAREDI na kuimba nyimbo za
ibada ya kikristo.
Wakati
alipo kuwa akiongea na wanafunzi wa, katika hafla fupi ya kuwakaribisha
kidato cha tano mnamo tarehe 28/4/2006 Pia alitamka wazi wazi kuwaambia
wanafunzi waislamu kuwa hapa shuleni hakuna kuswali swala tano kwani hii siyo seminari.Mnamo tarehe 18/06/2006 aliwaambia wanafunzi wa kiislamu wanaovaa
mavazi
yanayotambulisha uislamu wao, kama Kofia, Kanzu na Kilemba lau kama
angeliwajua asingewachagua kujiunga na shule yake.Mnamo tarehe
02/08/2006 aliwaita waislamu wanaovaa mavazi ya kiislamu kama kanzu kuwa
ni Mashoga
NDUGU WANAHABARI CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM)
Madhila
haya na manyanyaso hayawasibu wanafunzi wa kiislam waliopo mashule tu
lakini hata wale waliopo vyuo na vyuo vikuu pia hawajasalimika hapa
tutatoa mfano wa chuo kimoja tu cha Dodoma (UDOM)
ambako
wanafunzi wa kiislam chuoni hapo wamekuwa wakidhalilishwa, kwa
kutukaniwa dini yao na mtume wao mfano wa haya ni mwaka jana wakati wa
kampeni za uchaguzi wa serikali ya wanafunzi ambapo yalibandikwa
matangazo yenye ujumbe unaowatukana na kukejeri uislam na waislam kuwa
ni watu wasioweza na wasiostahiki kuongoza,jambo ambalo liliwafanya
wanafunzi wakiislam chuoni hapo kuripoti katika uongozi wa chuo na
vyombo vya usalama bila ya kupewa msada, hatimae waislam waliamua kujitowa
katika mchakato huo wa kampeni na uchaguzi wakiwa na nia njema ya
kujiepusha na uadui na uhasma baina yao na wanafunzi wa dini zingine,
lakini hata hivyo baada ya uchaguzi walitukanwa na
kukashifiwa
wazi wazi na wakirsto wakishangilia kwa kusema Yesu ameshinda na
Mohammad ameshindwa katika kona zote za chuo, bila ya kuchukuliwa hatua
za kisheria na mamlaka husika za chuo na serikali.
NDUGU WANAHABARI
Tukio
kubwa na la kusikitisha kwa wakati huu ni hili la shule ya sekondari
NDANDA iliyopo mkoa wa MTWARA wilaya ya Masasi tarafa ya Chikundi kata
Mwena kijiji cha Ndanda. Mpaka hivi sasa tunapozungumza nanyi wanafunzi
ishirini (20) wa kiislamu wamefukuzwa shule watano (5) wakiwa ni kidato
cha tano na kumi na tano ni kidato cha sita ambao wanatarajiwa kufanya
mtihani wa mwisho mwanzoni mwa mwezi wa pili.Aidha wengine waliosalimika
kufukuzwa shule wamewekewa masharti magumu ya
kusaini ikiwa wanataka kuendelea na shule hiyo ya serikali.Miongon mwa
masharti hayo ni kutojihusisha na dini yao wakiwa shuleni sharti ambalo
linapora haki ya kikatiba ya kuabudu.Sababu na kosa la kufukuzwa
wanafunzi hao wa kiislam likiwa ni kuuomba uongozi wa shule uwape eneo
maalumu la kufanyia ibada (Msikiti) kama vile walivyotengenezewa
wanafunzi wakirsto kanisa kubwa shuleni hapo,kulalamika lugha za kashfa
na dharau ambazo zinatolewa na mkuu wa shule dhidi ya wanafunzi wa
kiislamu uislamu shuleni hapo.
Kilichowaponza
wanafunzi waislamu ni kupinga udini wa mkuu wa shule na upendeleo kwa
wanafunzi wakristo, mfano kitendo cha mkuu wa shule kuteua viongozi wa
serikali ya wanafunzi kiholela na kiupendeleo kwa wakirsto huku wakitoka
nje ya shule wakishangilia na kusema Muhammad ameshindwa katika
uchaguzi mwache bwana Yesu atawale shule!!! Haya yamefanyika mkuu wa
shule akiyaona bila ya hata kukemea na kuwaadabisha wanafunzi wahusika jambo ambalo linaonesha wazi wazi kuwa ni mpango maalum ulio sanifiwa kwa mfumo maalum.
NDUGU WANAHABARI
TAMSYA
mikoa, wilaya na matawi, shule na vyuo kwa muda mrefu imefanya jitihada
mbalimbali za kuonana na wakuu wa shule na watendaji husikaNkatika
kadhia hizi na kuishia kupuuzwa bali na kupewa majibu ya kejeli na
jeuri. Na baadhi ya wakuu wa shule kuomba msamaha na kuahidikutorudia
tena, lakini baada ya muda mfupi hurejea na kuendeleza dhulma na madhila
kwa wanafunzi wakiislam kwa kasi ya ajabu.
Pia
walimu walezi wa wanafunzi wa kiislamu au hata walimu waislamu wanao
thubutu kuhoji juu ya ubaguzi wa kidini pia huonekana vioja huku
wakichekwa na hatimae kupewa adhabu ya kuhamishwa kituo cha kazi
kiholela mfano dhahiri ni walimu wawili pekee wakiislam wa Ndanda
Sekondari ambao wamefungashiwa virago vyao na kupelekwa vijiji vya mbali
kosa lao likiwa ni kutaka haki itendeke baina ya wanafunzi wote,na
wakati mwingine walimu waislam hujikuta wakiambulia vichapo na vipigo
kama alivyofanyiwa mwalim Halima wa Ifunda sekondari pale alipopinga
dhulma, uonevu na udhalilishwaji dhidi ya wanafunzi waislam shuleni hapo mwaka 2009 akajikuta anaambulia kipigo kutoka kwa mwalim wa kikristo.
NDUGU WANAHABARI
Hapa
tumeonesha sehemu ndogo ya madhila yanayowasibu wanafunzi wa kiislam
nchini kama mifano tu. kwani ni vigumu kueleza madhila ya kila shule au
chuo kwa njia hii. Jambo la faraja ni kuwa kila mtanzania
anajua haya hata watu wa kawaida pia Kwa kuwa tatizo hili ni la muda mrefu na baadhi ya viongozi wa serikali
mfano Rais mstaafu wa awamu ya Tatu Mh. Benjamin Mkapa alipoulizwa juu
ya hali ya uwiano wa waislamu na wasiokuwa waislam katika sekta ya elimu
alikiri kuwepo matatizo na uduni kwa upande wa waislam na matatizo mengi huku akisema kuwa si kosa la serikali bali ni tatizo la kihistoria.
Sisi
wanafunzi wa kiislam Tanzania tunasema wazi na tunao ushahidi kuwa hili
si tatizo la kihistoria bali ni mpango maalum uliosanifiwa na serikali
ya awamu ya kwanza kwa lengo la kuwadhulumu na
kuwakandamiza
waislam kielimu kwa mbinu mbalimali kama hizi zilizotumiwa na uongozi
wa shule ya sekondari Ndanda na wanaharakati wengine wa mfumo kiristo
katika sekta zote za elimu nchini.Wanafunzi wa kiislamu Tanzania tunajua
kuwa kitendo kilichokifanywa na mkuu wa shule ya Ndanda na Bodi ya
shule pamoja na maafisa elimu cha kuwafukuza shule wanafunzi ishirini
(20) wa kiislam na wengine
kuwekewa
masharti magumu ya kuacha wito wa dini yao ili waruhusiwe kurudi
shuleni si kitendo kipya bali ni muendelezo wa dhulma ambayo walifanyiwa
babu na baba zetu ambapo walilazimishwa wachague aidha
kuacha
dini au kusoma, Alhamdul llah tunashukuru kwa kiasi Fulani walifanya
maamuzi magumu ya kulazimika kuacha kusoma na kubaki na dini yao kwani
kama wangechagua la pili basi huenda nasi leo tusingekuwa katika dini ya haki ya uislam. Ama leo hii sisi wanafunzi wa kiislamu Tunasema kusoma ni sehemu ya dini
yetu kama tulivyoamrishwa na Allah (sw) Quran (96:1-5) kwa hiyo
hatutokubali tena kuacha wito wa dini yetu kwa kutenganisha dini na
elimu kwani ikiwa tutafanya hivyo basi itakuwa tumefanya dhulma kubwa kabisa.
Hapa tunawapongeza wanafunzi wa kiislam wa Ndanda sekondari kwa
kujitambua na kujua haki zao za kiiman na kikatiba kwa kutoutii uongozi
wa kidhulma wa shule ya ndanda pale ulipowalazimisha kuacha wito
wa dini yao ili wasome, wanafunzi wa Ndanda wamefanya jambo tukufu
linalopaswa kuungwa mkono na kuigwa na kila mtu mwema. Na napenda kutoa
wito kwa wanafunzi wakiislam nchini kote ya kuwa wanapaswa kuwaiga na kuungana na ndugu zao zao wa Ndanda sekondari kwa kutokubali dhulma ya namna yoyote ile.
NDUGU WANAHABARI
Kadhia
ya Ndanda ni mzito sana ambayo imegusa hisia ya kila muislam na kila
mtanzania mpenda amani na haki, ukweli wa hili unathibitika wazi wazi
kwa kila mwenye uhuru wa kufikiri kwani vijana wale wa kidato cha sita
waliofukuzwa ni nguvu kazi muhimu sana kwa ujenzi wa taifa ambao tayari
kusoma kwao wangeweza kuiokomboa jamii na taifa kiujumla.Lakini jambo la
kusikitisha ni kuona viongozi wenye dhamana katika wizara
ya elimu wakilichukulia swala hili kisiasa kinyume na uhalisia wake.
Kwa kufanya ziada na uchunguzi wa kubahatisha bila umakini hatimae kutoa
taarifa zilizojaa usiasa ndani yake, kuwa eti maamuzi ya bodi
ya kuwafukuza wanafunzi (20) wa kiislam ni sahihi huku akieleza kuwa
amefika Mtwara na kuongea na Bodi ya shule, mkuu wa shule, walimu na
serikali ya wanafunzi hatimae wanafunzi wote Paredi bila ya kuwaruhusu
kuuliza maswali au kutoa maoni yao hatimae kutoa hukumu.Hukumu hii
haiwezi kuwa sahihi kwani hajawashirikisha wahusika wa upande wa pili wa
mgogoro ambao ni wanafunzi wa kiislam kwa kuwasikiliza
hoja zao madai yao ya msingi, huku ni kuisaliti katiba ambayo wameapa
kuilinda ambayo inarususu uhuru wa kutoa mawazo na kila mmoja
kuheshimiwa kwa nafasi yake. Jambo zito zaidi ni kuona naibu waziri
anaungana na watu madhalimu waliovunja katiba ya nchi kwa kuwalazimisha
wanafunzi kuacha wito wa dini yao ili warudi shule sharti hili linavunja
katiba Ibara ya (19:1-2) kinachozungumzia uhuru
wa imani na kuabudu.Kutokana na uzito na unyeti wa kadhia hii na madhila haya yanayoendelea
kufanywa dhidi ya wanafunzi wa kiislam nchini leo hii tunapenda
tuutangazie uma kuwa sasa basi hatutaki kuendelea tena kudhulumiwa na
kunyanyaswa, sisi ni watanzania na tuna haki zote kama wanajamii wengine.Kwahiyo tumeitaka serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kufanya mambo yafuatayo;
Tunaitaka wizara ya elimu kuwarejesha wanafunzi wote walofukuzwa na
wengine bila masharti yeyote ndani ya siku tano (5) kuanzia tarehe
13/01/2012.
Tunaitaka serikali kuunda Tume huru itakayo chunguza kero wanazopata wanafunzi waislamu katika shule za serikali nchi nzima.
Tunaitaka serikali kuwawajibisha watendaji wa sekta ya elimu
wanaoendekeza udini ubaguzi na unyanyasaji kwa wanafunzi wa kiislamu.
Tunaitaka serikali ithibitishe au ikanushe juu ya madai ya mkuu wa
shule Ndanda na badhi ya viongozi wa serikali kuwa mashule
yaliyotaifishwa na serikali, serikali inamiliki majengo tu ama ardhi
na mamlaka ya matumizi yake yako chini ya Taasisi zake za asili.
Shule zote za serikali zitenge maeneo malum ya kufanyia ibada kwa
ajili ya watu wa dini zote. Asilimia kubwa ya wakuu washule za sekondari za serikali ni wakristo, hivyo basi tunaomba serikali iweke mgawanyo sawa wa nafasi hizo.
Kila
jambo linapaswa kuwa na mwisho, hatuwezi kuendelelea kuvumilia uonevu
wa wazi wazi siku zote.Hatuwezi tena kuendelea kuishi kama wanafunzi
daraja la pili katika nchi yetu.Lazima haki sawa na uhuru upatikane kwa
wanafunzi wa dini zote na sio kukandamiza waislamu. Hivyo basi
tunalazimika kupaza sauti zetu kwaNkuingia barabarani kuonesha hisia
zetu katika hali ya unyonge wetu
NDUGU WANAHABARI
Tunakusudia
kufanya maandamano ya amani nchi nzima 20 Januari 2012 ambayo
yatapeleka ujumbe kwa kila kiongozi wa Elimu katika mkoa yaani Afisa
Elimu Mkoa na waislam wa Mkoa wa Dar es salaam watapeleka ujumbe moja
kwa moja kwa waziri wa elimu.Kwa lengo la kutaka azingatie madai yetu ya
kutonyanyaswa na kubaguliwa katika shule ya serikali.Lakini hatutoishia
katika maandamano iwapo hali ya ubaguzi haitokoma.Tutatumia
njia nyingine za kujikomboa katika madhila
haya.Tunasema“tumenyanyaswa, tumedhaliliswa, tumebaguliwa kwa miaka 50 ya
uhuru na tukavumilia na kusubiri vyakutosha leo tunasema inatosha na
tumechoka tunaitaka serikali itambue haki,heshima na utu wetu kama
wanavyoheshimiwa wanafunzi wa dini zingine mashuleni na
mavyuoni.”Tunataka tuheshimiwe kama wanaadamu, kama wanatanzania huru,
wanafunzi halali mashuleni na vyuoni kama wananyoheshimiwa wanafunzi wa
dini zingine. Tumeanza muda mrefu kudai haki zetu kwa njia za
kidiplomasia lakini hatujasikilizwa na leo tunatumia njia nyingine ya
kidiplomasia na kikatiba ambayo ni MAANDAMANO ya amani huenda kwa njia
hii serikali na jamii itasikia kilio chetu.
ACHENI KUTUDHALILISHA NA KUTUNYANYASA WANAFUNZI WA KIISLAM MASHULENI NA MAVYUONI SASA BASI INATOSHA TUNAOMBA WAISLAM WOTE NA WAPENDA AMANI WOTE MTUUNGE MKONO KATIKA MAANDAMANO HAYA YA AMANI.
Ahsanteni. JAFARI SAIDI MNEKE RAISI WA JUMUIYA YA WANAFUNZI NA VIJANA WA KIISLAMU TANZANIA (TAMSYA)
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)