TAARIFA KWA UMMA NA VYOMBO VYA HABARI
TAHADHARI YA ONGEZEKO LA MVUA MAENEO YA KUSINI
MWA NCHI.
--
Msimu wa mvua unaendelea katika maeneo yanayopata mvua mara moja kwa
mwaka (mikoa ya Mtwara, Lindi, Ruvuma, Mbeya, Iringa, Morogoro kusini,
Rukwa, Dodoma, Singida, Kigoma na Tabora.)
Katika
kipindi cha siku tano kuanzia Januari 5 hadi Januari 10, 2012,
mgandamizo mdogo wa hewa katika eneo la rasi ya Msumbiji unatarajiwa
kuendelea kuimarika hivyo kusababisha ongezeko la mawingu katika maeneo
ya kusini mwa nchi.
Hali hii
inatarajiwa kuimarisha makutano ya upepo wenye unyevunyevu katika
maeneo hayo, hivyo kusababisha vipindi vya mvua kubwa katika maeneo ya
Nyanda za juu kusini magharibi (mikoa ya Iringa, Mbeya na Rukwa), maeneo
ya kusini (mikoa ya Ruvuma, Mtwara na Lindi), baadhi ya maeneo ya
Kusini mwa mkoa wa Pwani na Kusini mwa mkoa wa Morogoro (Mahenge).
Aidha
mvua za kawaida za masimu zinatarajiwa kuendelea kunyesha katika
maeneo ya kanda ya kati (Mikoa ya Dodoma na Singida) na magharibi mwa
nchi (Mikoa ya Kigoma na Tabora).
Maeneo ya Pwani ya kaskazini ( mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani na visiwavya Unguja na Pemba), baadhi ya maeneo ya Nyanda za juu kaskazini masharikiyanatarajiwa kuwa na vipindi vya mvua ambazo ziko nje ya msimu.
Mvua hizi zinatarajiwa kuambatana na upepo mkali katika maeneo ya Bahari yaHindi, hivyo watumiaji wa Bahari wanashauriwa kuchukua tahadhari.
Mamlaka ya Hali ya Hewa inaendelea kufuatilia mwenendo wa mifumo ya Hali yahewa na athari zake na itaendelea kutoa taarifa.
IMETOLEWA NA
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)