Serikali ya Iran Yatenga Dola Milioni 5 Kujenga Chuo cha Ufundi Zanzibar - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Serikali ya Iran Yatenga Dola Milioni 5 Kujenga Chuo cha Ufundi Zanzibar

Waziri wa Elimu wa Zanzibar Ramadhan Abdalla Shaaban
--
Na Fatma Mzee-Maelezo Zanzibar
.
Jumla ya Dola Milioni Tano zimetengwa na Serikali ya Iran kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa Chuo cha Ufundi Zanzibar ikiwa ni hatua ya kwanza ya ujenzi huo.Yameelezwa hayo na Mshauri wa Rais wa Mambo ya Utamaduni Nchini Iran Bw Sher Salahi huko Wizara ya Elimu alipokuwa akizungumza na Waziri wa Elimu wa Zanzibar Ramadhan Abdalla Shaaban huko Afisini kwake.

Amesema yeye pamoja na Ujumbe aliofuatana nao wamekuja kufuatilia makubalianao yao na kuona eneo ambalo limeshatengwa kwa ajili ya kazi hiyo kwa vile wako tayari kuanza kazi hiyo ya ujenziNaye Waziri wa elimu alieza kuwa kiwanja hicho ambacho kipo eneo la Tunguu bado kina malengo yale yale yalio kusudiwa hivyo kama Serikali ya Iran iko tayari ni vyema kuja kuanza ujenzi huo.

Amesema kuwa hiyo ni nafasi nzuri kwa Zanzibar kwani mbali ya kutoa taaluma itaweza kutoa ajira kwa vijana.Aidha Waziri aliushauri ujumbe huo kuunda kamati amabayo itakuwa na kazi ya kuratibu na kufuatilia utekelezaji wa mradi huo.

Mapema ujumbe huo ulipata nafasi ya kutembelea Afisi ya Nyaraka iliyopo Kilimani Mjini Zanzibar na kuweza kujionea jinsi nyaraka hizo zinavyo hifadhiwaChuo hicho kitakapomalizika kujengwa kinatarajiwa kusomesha mambo ya kuhifadhi Nyaraka kwa lengo la kuwa na Walimu na Wafanya kazi wenye uwezo wa kisasa wa kuhifadhi Nyaraka na kuweka kumbu kumbu kwa utaalamu zaidi.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages