Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akipokea msaada
wa flana maalumu zitakazo tumika kwenye Sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar
zilizotolewa na Kampuni ya Bia ya Serengeti Breweries (SBL) kupitia
kinywaji chake cha Malta Guinness leo, anayekabidhi ni Mkurugenzi wa
Mawasiliano wa SBL, Teddy Mapunda.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa SBL, Teddy Mapunda
(kushoto) akizungumza kabla ya kukabidhi msaada wa flana 2000 zenye
thamai ya sh milioni 15, anayesikiliza katikati ni Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, kulia ni Waziri wa nchi Ofisi ya
Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud.
Na Joachim Mushi, Zanzibar
KAMPUNI ya Bia ya Serengeti Breweries (SBL) kupita
kinywaji chake kisicho na kilevi cha Malta Guinness wametoa msaada wa
flana maalumu kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) zitakazotumika
katika Maadhimisho ya Sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar.
Mapunda amesema SBL inaungana na SMZ pamoja na Wazanzibari wote
katika kusherehekea siku kuu ya Mapinduzi, ambazo huadhimishwa kila
ifikapo Januari 12, ya kila mwaka.
Amesema flana hizo 2,000 zinazogharimu sh. milioni 15 zitatumika
katika maadhimisho ya sherehe hizo maalumu zinazofanyika kesho mjini
hapa. SBL imesema itaendelea kushirikiana na SMZ katika masuala
mbalimbali ya kijamii ikiwa ni ada ya kampuni hiyo ya kuisaidia jamii
kupitia shughuli anuai za kijamii.
Naye Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd
akipokea msaada huo amsesema anaishukuru kampuni hiyo kwa msaada wao na
kuiomba isiishie hapo katika kuisaidia Zanzibar.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)