Na.Faki Mjaka – Maelezo Zanzibar
Ripoti
ya Tume ya kuchunguza ajali ya kuzama kwa Meli ya Mv. Spice Islanders 1
imependekeza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Mustafa Aboud Jumbe
pamoja na wahusika wengine wachukuliwe hatua za kisheria na kinidhamu
kutokana na uzembe waliofanya na kusababisha kuzama kwa Meli hiyo
Akitoa
mapendekezo ya Ripoti hiyo leo katika Ukumbi wa Wizara ya Habari Katibu
wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Katibu Mkuu Kiongozi Abdulhamid
Yahya Mzee amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeyakubali
mapendekezo ya ripoti hiyo na kusema itaiachia Mahaka na Jeshi la Polisi
kutimiza wajibu wao
Dk.Abdulhamid
amesema miongoni mwa watu ambao walibainika na makosa katika ajali hiyo
ni pamoja na Mkurugenzi wa Mamalaka ya Usafiri wa Baharini Zanzibar
Haji Vuai Ussi,Mkuu wa kituo cha usimamizi wa usalama wa vyombo vya
baharini wa Shirika la Bandari,Usawa Khamis Said na Kaimu Mdhibiti wa
Bandari ya Malindi Sarboko Makarani Sarboko.
Wengine
ni pamoja na Wanahisa wa Kampuni inayomiliki meli hiyo Jaku Hashim Ayub
ambaye ni Mwakilishi na Mbuge wa Jimbo la Muyuni,Salim Said Mohammed,
Makame Hasnuu Makame na Yussuf Suleiman Issa.
Dk.Abdulhamid
amesema wahusika wote waliotajwa katika ripoti hiyo ikiwa ni pamoja na
Captain wa Meli hiyo Said Abdallah Kinyanyite na wasaidizi wake,Afisa
usafirishaji wa Shirika la Bandari Hassan Mussa Mwinyi na Mkaguzi wa
Meli wa Mamlaka ya Usafisiri wa Baharini Juma Seif Juma watachukuliwa
hatua za kisheria kulingana na makosa yao
Mrajis
wa meli Abdallah Mohammed Abdallah, Afisa Usalama wa Mamlaka ya Usafiri
wa Baharini Simai Nyange Simai, na wasimamizi wa watatu wa uingiaji wa
abiria katika meli hiyo Yussuf Suleiman Issa,Shaib Said Mohammed na Juma
Abdallah Hussein nao wachukuliwe hatua za kisheria na kinidhamu.
Wengine
ni Afisa Mkuu wa Mv.Spice Abdalla Mohammed Ali,Mhandisi Mkuu wa Meli
hiyo Khamis Ahmada Hilika, Mabaharia wote wa Meli hiyo pamoja na Askari
wa Bandarini waliokuwepo zamu katika kupanga abiria siku ya tukio ambao
ni Sajent Jumbe Muhaji na Koplo Juma Abdulla.
Akizungumzia
juu ya fidia kwa wahanga wa ajali hiyo Dk.Abdulhamid amesema jukumu la
kuwalipa wahanga hao liko mikononi mwa wamiliki wa meli hiyo kwa mujibu
wa sheria na kwamba vigezo vya kulipwa wahanga vitafuata utaratibu
maalum uliowekwa ambapo kwa waliofariki watalipwa si chini ya Sh Milioni
Kumi
Kwa
waliopata ulemavu watalipwa asilimia 75% ya Fedha watakazolipwa
waliofariki dunia ambapo waliokuwemo katika meli hiyo bila kupata
ulemavu watapata asilimia 50% ya kiwango hicho.
Kuhusu
fedha za michango ya maafa ambazo zimetolewa na taasisi mbalimbali Dk.
Abdulhamid amesema fedha hizo zitagawiwa kwa wahusika chini ya utaratibu
maalum utakaowekwa na Mfuko wa Kamati ya maafa uliopo chini ya Afisi ya
Makamu wa Pili wa Rais
Aidha Dk.Abdulhamid alisema ripoti hiyo itawekwa wazi na kupatikana katika mitandao na Maktaba kuu ili wananchi waweze kuisoma.
Ripoti
ya Tume hiyo iliundwa na Rais waZanzibarna Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kufuatia kuzama kwa Meli ya Mv. Spice
Islanders 1 tarehe 9/09/2011 katika Mkondo wa Nungwi kuelekeaPembaambapo
inasadikiwa ilikuwa na abiria 2470 na tani kadhaa za mizigo





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)