Ali Kiba (kushoto) akiwa na backup singer wake Abdul Kiba
wakitumbuiza umati wa washabiki wakikomoro waliojitokeza kuja kumwona mtunzi wa
‘Dushelele’ uwanjani hapo.
Precision Air ndio waliokuwa wanadhamini wakuu wa
show hiyo iliyoandaliwa na mapromota wa East Africa Tour wa jijini Comoros.
Precision Air – Shirika la ndege linaongoza nchini hivi
karibuni ilidhamini show ya nguvu ya mwanamuziki Ali Kiba iliyofana jijini
Moroni, Comoros.
Akiwa jijni Moroni, Afisa Mawasiliano wa kampuni hiyo Bw.
Amani Nkurlu alisema kwamba sababu ya kudhamini show hiyo ni kuwakumbusha soko
la Comoros kwamba shirika la ndege hiyo ipo pamoja nao si tu kibiashara bali
hata katika mambo ya kijamii, ikiwa na kupokea mwaka mpya kwa furaha na
shangwe. “Pamoja na hayo,
kudhamini show hii ni kama njia moja yapo pia ya kukuza muziki wakitanzania na
kuwatangaza wanamuziki wetu nje ya nchi,” alisema Nkurlu.
Kwa upande wake, mwanamuziki wa kizazi kipya Ali Kiba
alielezea kwamba show ya Comoros imeweza kwenda vizuri sana na kwamba washabiki
wa huko wameweza kuonyesha mapenzi ya dhati kwa muziki wa kitanzia.
“Comoros ni nchi wanaotumia lugha ya kifaransa na kingazidja
kwa wingi, ni wachache tu wanaoweza kuzungumza Kiswahili kwa ufasaha. Lakini cha
ajabu ni kwamba umati huu umeweza kuimba mstari baada ya mstari wa nyimbo zangu
karibia zote,” alisema Kiba baada ya show.
Aliongeza, “Hili ni
jambo la kutia moyo sana, na ninawashukuru washabiki wangu wa Comoros kwa hili,
waandaaji na kampuni ya Precision Air kwa yote.”
Show hiyo iliyohudhuriwa na watu zaidi ya elfu 3 iliandaliwa
na mapromota wa East Africa Tour kutokea jijini Moroni, Comoros. Hahaya - Moroni
ni moja ya sehemu 15 ambazo Precision Air iendapo ukiondoa Dar es Salaam,
Kilimanjaro, Kigoma, Musoma, Mtwara,
Mwanza, Tabora, Shinyanga, Bukoba, Zanzibar,
Entebbe, Nairobi, Johannesburg, Mombasa.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)