MABONDIA MANENO OSWARD NA RASHIDI MATUMLA KUPAMBANA TENA BAADA YA KUTOKA SARE - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MABONDIA MANENO OSWARD NA RASHIDI MATUMLA KUPAMBANA TENA BAADA YA KUTOKA SARE

Promota wa mpambano wa ngumi, Issa Malanga (kushoto) akitiliana saini mkataba na bondia Maneno Osward kwa ajili ya mpambano wake dhidi ya bondia Rashidi Matumla litakalofanyika Februar 25 katika ukumbi wa PTA Sabasaba. Picha kwa hisani ya superd boxingcoach.blogspot.com


                                                                             ******************************************

MAANDALIZI ya pambano lisilo la ubingwa kati ya mabondia Rashid Matumla ‘Snake Man’ na Maneno Oswald ‘Mtambo wa Gongo’ lililopangwa kuwa Februari 25 mwaka huu yanaenda vizuri.

Promota wa mpambano huo Issa Malanga, alisema pambano hilo limeandaliwa ili kumaliza ubishi baina ya mabondia hao, ambao pambano la mwisho walitoka sare ya point 99.99

Hata hivyo Oswald aliwalalamikia majaji kuwa hawakumtendea haki. Mabondia hao wamewahi kupambana mara nne, Oswald akishinda mara moja na Matumla mara mbili na kutoka sare mara moja.

Alisema pambano hilo linatarajia kuwa la raundi 10 uzito wa kati, litafanyika kwenye ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam

Mpambano huo wa kumaliza ubishi baada ya kila mmoja wao kudai alishinda katika mpambano wao wa mwisho

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages