Msanii Nguli wa sanaa za
maonesho, Bakari Kassim Mbelemba (Mzee Jangala) aikizungumza na wadau wa sanaa
kwenye Jukwaa la Sanaa linaloendeshwa na BASATA kila siku ya
jumatatu.Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya ukuzaji sanaa, BASATA Vivian
Shalua
Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Sanaa ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idaya ya Ukuzaji Sanaa, Bi. Shalua akifafanua jambo wakati akihitimisha mjadala kuhusu Sanaa za majukwaani kwenye Jukwaa la Sanaa wiki hii. Kushoto ni Mzee Jangala na Kaimu Mratibu wa Jukwaa la Sanaa, Aristide Kwizela.
Mdau wa Sanaa akitaka ufafanuzi juu ya masuala mbalimbali yahusuyo Sanaa za majukwaani.
Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Sanaa ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idaya ya Ukuzaji Sanaa, Bi. Shalua akifafanua jambo wakati akihitimisha mjadala kuhusu Sanaa za majukwaani kwenye Jukwaa la Sanaa wiki hii. Kushoto ni Mzee Jangala na Kaimu Mratibu wa Jukwaa la Sanaa, Aristide Kwizela.
Mdau wa Sanaa akitaka ufafanuzi juu ya masuala mbalimbali yahusuyo Sanaa za majukwaani.
Sehemu ya
wadau waliohudhuria katika Jukwaa la Sanaa wakifuatilia
mjadala.
Na: Mwandishi wetu
Msanii nguli wa Sanaa za Maonesho,
Bakari Kassim Mbelemba (Mzee Jangala) amesema kuwa programu ya Jukwaa la Sanaa
inayoendeshwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ni chuo tosha kwa wasanii
katika kuwapa elimu na ufahamu wa masuala mbalimbali ya sekta ya
Sanaa.
Akizungumza wiki hii, kwenye programu
hiyo katika ukumbi wa BASATA, Ilala Sharif Shamba, Jangala alisema kuwa, Jukwaa
la Sanaa ni jambo la kujivunia na ni chachu ya kukua kwa Sanaa.
“Jukwaa la Sanaa ni programu
inayonifanya nithubutu kusema, sasa Sanaa ni kazi, maana kazi yoyote ili ifanywe
kwa ufanisi inahitaji elimu, uratibu na mwongozo, hivyo wasanii tuitumie fursa
hii adimu” Jangala alisema.
Aliongeza kuwa, programu hii imekuwa
ikiwaleta wataalam na wadau mbalimbali wenye uzoefu katika sekta ya Sanaa hivyo,
kwa wasanii ambao wamekuwa wakihudhuria toka mwanzo wamepata mambo mengi ambayo
yatawasaidia katika kukuza na kuendeleza vipaji vyao.
Alisisitiza kuwa, Sanaa inabadilika
na kumezwa na teknolojia mpya zinazokuwa zinajitokeza hivyo, ni lazima wasanii
wajenge utamaduni wa kutafuta maarifa mapya na kuwa wabunifu huku wakizingatia
maadili ya kitanzania.
Kuhusu wasanii kulewa umaarufu na
sifa, alishauri kuwa ni vema wakabadilika na kufanya kazi zao kwa bidii na
ubunifu zaidi kwani, sifa ya msanii inakuja yenyewe kutokana na kazi
anazozalisha na kupeleka kwa jamii inayomzunguka.
“Sifa ya mpishi hutolewa na mlaji,
kwa hiyo wasanii wanapotengeneza kazi zao wasijisifu wenyewe bali wasubili
kusifiwa na msikilizaji au mtazamaji” alishauri Mzee Jangala.
Alizungumzia pia suala la wasanii
kutegemea vipaji tu pasipo kuingia darasani na kusema kuwa hilo haliwezi kukuza
sekta ya sanaa na badala yake tutakuwa na kazi zinazoandaliwa kwa msukumo wa
soko na si taaluma ya Sanaa
“Wasanii ni lazima watambue kuwa,
mbolea ya kipaji chochote kile ni elimu. Ni vigumu sana kutegemea kipaji tu
pasipo kukipalilia kwa taaluma ya sanaa husika”
Kwa upande wake, kaimu mwenyekiti wa
Jukwaa la Sanaa, Vivian Nsao Shalua alishauri wasanii kulitumia Jukwaa la Sanaa
ili kuzijua sheria, taratibu na mbinu mbalimbali zitakazo waongoza
katika shughuli zao za Sanaa.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)