Askari wa Bunge wakibeba Jeneza kuelekea mahala palipoandaliwa rasmi kwa ajili ya shughuli za kuaga
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akisalimiana na kuagana na Andrew Chenge pamoja na baadhi ya
wananchi waliohudhuria shughuli hiyo ya kuaga mwili wa marehemu Regia,
wakati akiondoka katika viwanja hivyo vya Karimjee, leo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akisalimiana na kuagana na Tundu Lissu, Vita Kawawa, pamoja na
baadhi ya wananchi waliohudhuria shughuli hiyo ya kuaga mwili wa
marehemu Regia, wakati akiondoka katika viwanja hivyo vya Karimjee,
leo.
Mke
wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Zakhia
Bilal, Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda, Waziri wa Afrika Mashariki,
Samuel Sitta na Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, wakiwa katika
shughulia ya kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA,
marehemu Regia Mtema, aliyeagwa leo katika Viwanja vya Karimjee jijini
Dar es Salaam. Regia anatarajia kuzikwa kesho nyumbani kwao Ifakara.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania, Anne Makinda Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,Naibu Spika Job Ndugai na
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, wakiwa katika shughulia ya kuaga
mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA, marehemu Regia Mtema,
aliyeagwa leo katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Regia
anatarajia kuzikwa kesho nyumbani kwao Ifakara.
Makamu
Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal
na mkewe Mama Zakhia Bilal, wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa
aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia CHADEMA, marehemu Regia Mtema,
aliyefariki mwishoni mwa wiki kwa ajali ya gari eneo la Daraja la Mto
Ruvu. Mwili wa marehemu Regia umeagwa leo Januari 17, katika Viwanja vya
Karimjee jijini Dar es Salaam na kusafirishwa kuelekea nyumbani kwao
Ifakara kwa maziko.
Spika
wa Bunge, Anne Makinda, akitoa wasifu wa mare hemu katika shughuli zake
za kibunge na salam za rambirambi kwa niaba ya Bunge.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akitoa salama za rambirambi kwa niaba ya Serikali.Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi ya Makamu Wa Rais
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)