Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar na Mbunge wa Kitope Balozi
Seif akimkabidhi sare ya skuli mmoja wa wanafunzi wanaoishi katika
mazingira magumu wa skuli nn zilizomo ndani ya jimbo lake. Hafla hiyo
fupi imefanyika katika viwanja vya skuli ya kitope ikiwashirikisha pia
wafadhili wa msaada huo kutoka Uniform Tanzania Bibi Agnes Sjoberg Na
Bibi Sophie Mellstig.
Mbunge
wa Jimbo a Kitope na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali
Iddi akimkabidhi madeski ya ukumbi wa mikutano wa skuli ya kitope
Mwalimu Mkuu wa Skuli hiyo Mwalimu Kombo Madeski hayo 70 yaliyotolewa na
washirika wa maendeleo yana thamani ya shilingi milioni 5,000,000/-.
Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar
na Mbunge wa Kitope Balozi Seif Ali Iddi akiwa katika picha ya pamoja
na walimu na baadhi ya wajumbe wa kamati za skuli za jimbo la kitope
pamoja na washirika wa maendeleo bibi agnes sjoberg na bibi sophie
mellstig mara baada ya hafla ya kukabidhi madeski na sare kwa wanafunzi
wenye mazingira magumu jimboni kitope.
--
Mbunge
wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi amesema ni vyema kwa Wanafunzi
kuzingatia kuwa misaada inayotolewa na Washirika wa Maendeleo inakuwa
chachu kwao katika kujitafuatia elimu itakayowafaa hapo baadaye.
Balozi
Seif ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema hayo
katika hafla fupi ya kukabidhi vikalio 70 kwa ajili ya ukumbi wa Skuli
ya Kitope pamoja na sare 222 kwa wanafunzi wa skuli nne za Jimbo hilo
wanaoishi katika mazingira magumu.
Hafla
ilifanyika katika Viwanja vya Skuli ya Kitope ambapo Vikalio
hivyovimetolewa na Washirika wa Maendeleo vikiwa na Thamani ya Shilingi
Milioni 5,000,000/- wakati sare zilifdhiliwa na Taasisi ya Uniform
Tanzania zikiwa na Thamani ya shilingi Milioni 3,108,000/-.
Balozi
Seif alisema hatua ya Wanafunzi hao kusoma kwa bidii itawapa moyo
Wahisani pamoja na Washirika wa Maendeleo kuendelea kusaidia Sekta ya
Elimu hapa Nchini.
Mbunge
huyo wa Jimbo la Kitope amewapongeza Wafadhili hao kwa juhudi zao za
kuchangia Sekta ya Elimu ambayo ni muhimu kwa Kizazi kijacho kutokana na
mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia.
Akitoa
shukrani kwa Niaba ya Walimu na Wanafunzi wa Skuli zote zilizopata
msaada huo Msaidizi Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Kitope Nd. Suleiman Juma
Makame alisema bado wanaendelea kuthamini juhudi na misaada inayotolewa
na washirika pamoja na Viongozi wao.
Ndugu
Suleiman alisisitiza kwamba Jamii inayowazunguuka inafarajika kuona
lengo la Viongozi la kutaka kuimarisha sekta ya Elimu linatekelezeka.
Naye
Mmoja wa Wafadhili wa Sare za Wanafunzi hao wa Taasisi ya Uniform
Tanzania kutoka Nchini Sweden Bibi Agnes Sjoerg alisema lengo la Taasisi
yao ni kushajiisha elimu kwa vile ndio Mkombozi wa Mwanaadamu.
Bibi
Agnes alisema Wanachama wa Taasisi hiyo ambao ni Wanafunzi Nchin Sweden
wamefikia uamuzi wa kuchangishana kwa ia ya kusaidia Wanafunzi wenzao
Nchini mbali mbali ambazo zimekuwa na watoto wenye mazingira magumu.
Mapema
MBunge wa Jimbo la Kiope Balozi Seif Ali Iddi alikitembelea Kikundi cha
Ushoni cha Jimbo la Kitope Kinachoendelea kupata mafunzo ya ushuno hapo
katika Ofisi ya CCM jimbo la Kitope.
Balozi
Seif katika ziara hiyo aliambatana pamoja na Wawakilishi wa Uniform
Tanzania Bibib Agnes Sjobeg, Bibi Sophie Mellstig pamoja na Mkurugenzi
Mkuu wa chuo cha Ushoni Kiliopo Magomeni { Magomeni Modern Tailoring
Academy } Ndugu Rashid Makame Shamsi.
Akitoa
Salamu zake kwa wanakikundi hao wa Kitope Mkurugenzi huyo wa Modern
Tailonring Academy Nd. Rashid alisema uongozi wake utajaribu kuratibu
namna ya kutoa Mafunzo kwa Wanakikundi hao ili kuwasaidia zaidi Taaluma
ya Ushoni.
Hata
hivyo Nd. Rashid alitahadharisha kwamba mafunzo ya ya ushoni
yamebadilika na kuwa ya Kitaalamu zaidi jambo ambalo wana kikundi hao
wakubali kubadilika.
Alielezea
matumini yake kwamba mafunzo hayo mbali ya kutoa uelewa mkubwa zaidi
lakini pia yatasaidia kuipunguzia mzigo wa ajira Serikali Kuu kwa vile
wao watakuwa tayari wameshajihakikishia ajira ya kudumu.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
16/1/2012.
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
16/1/2012.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)