Enzi ya Uhai wake
Baada yakuugua kwa muda mrefu mpaka umauti
Mwigizaji
maarufu wa maigizo nchini aliyetambulika kwa jina la Mzee Kipara,
amefariki dunia leo saa mbili asubuhi maeneo ya Kigogo Mbuyuni baada ya
kuugua kwa muda mrefu. mwigizaji huyo ambaye amekuwa kama mlezi wa kundi
la Kaole, alikuwa akiishi hapoa katika nyumba ya kaole baada ya
kuchukuliwa na wasanii wenzake baada ya kuugua kwake.
Mwili
wa marehemu umepelekwa kuhifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala,
wakati wakijiandaa kwa mazishi kesho saa kumi. Fununu habari inawapa
pole wapenzi wake wote wa maigizo yake ndugu na jamaa ,waigizaj na
watanzania wote.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi......... Amin
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)