BONDIA ASHA NGEDELE WA DAR AMTWANGA SALMA WA MORO KWAO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

BONDIA ASHA NGEDELE WA DAR AMTWANGA SALMA WA MORO KWAO

 
Salma akipewa ushauri wakati wa mapumziko.
 
Kama wanacheza rhumba!
 
Konde kwa konde.
 
Asha (kushoto) akitangazwa mshindi.
Salma akimrushia Asha konde la kulia.
Hola!  Salma kakoswa konde la mauaji!


BONDIA wa kike, Asha Nzoha, a.k,a Asha Ngedere, wa jijini Dar es Salaam jana usiku alilipa kisasi baada ya kumtwanga kwa pointi mpinzake wake wa jadi, Salma Kihobwe, wa Morogoro katika mpambano uliofanyika katika manispaa hiyo ya ‘Mji Kasoro Bahari’.

Katika mpambano wa awali uliofanyika jijini Dar es Salaam, Salma aliibuka mshindi kwa kumchapa Asha mbele ya mashibiki wake, lakini jana bondia huyo alilipa kisasi kwa kumchapa Salma mbele ya mashabiki wake waliokuwa wakimshangilia kwa nguvu zote.

Baada ya majaji kutangaza matokeo hayo, Asha Ngedele aliruka kwa furaha huku Salma akipokea matokeo hao kwa kukunja mdomo kama mtu aliyeramba ndimu.   
 NA DUNSTAN SHEKIDELE,  GPL, MOROGORO

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages