Mkurugenzi
wa Idara ya Mfuko na Uwezeshaji, BASATA Angelo Luhala aksisitiza jambo
wakati akieleza haja ya Wasanii kudai mikataba kabla ya kushiriki tukio
au onyesho lolote la Sanaa.
Mkurugenzi Idara ya Ukuzaji Sanaa BASATA, Vivian Nsao Shalua akizungumza
na wadau wa Sanaa katika Jukwa la Sanaa linalofanyika kila wiki makao
makuu ya Baraza hilo. Kulia ni Afisa Habari wa BASATA Aristide Kwizela.
Mdau
wa Sanaa akichangia kwa hisia kali wakati wa mjadala uliohusu matukio
na matamasha mbalimbali ya Sanaa na Burudani nchini kwenye Jukwaa la
Sanaa.
Na Mwandishi Wetu
Baraza
la Sanaa la Taifa (BASATA) limewaonya wakuzaji sanaa nchini kuacha mara
moja ubabaishaji wanapokuwa wanaendesha matukio na matamasha mbalimbali
ya Sanaa.
Onyo
hilo limetolewa mapema wiki hii na Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Sanaa
wa Baraza hilo, Vivian Nsao Shalua wakati akiongea na wadau wa Sanaa
kwenye programu ya Jukwaa la Sanaa inayofanyika kwenye ukumbi wa BASATA
uliopo Ilala Sharifu Shamba.
Shalua
alisema kuwa, Mapromota wamekuwa wakiwarubuni wasanii kwa kuwafanyisha
kazi zisizo na mikataba huku wao wakinufaika na kuwaacha wasanii
wakishindwa kujikwamua kimaisha.
“Utaratibu
uliopo sasa kila mdau yeyote anapoandaa tamasha au tukio lolote
linalohusisha wasanii lazima aje na mikataba na wasanii hao, aoneshe
uwezo wake kifedha katika kuendesha tukio lakini pia awe na kamati
inayoeleweka ya uendeshaji” alisisitiza Shalua.
Aidha,
aliongeza kuwa, kumekuwa na ukiukwaji kanuni na taratibu za uendeshaji
matukio hayo ambapo Baraza limekuwa likiwapa onyo na kuwafungia wahusika
lakini akasisitiza kuwa, njia pekee ya kuepuka hali hii ni kwa
mapromota kufuata taratibu zilizopo.
Akizungumzia
kuhusu suala la mikataba, aliwataka Wasanii kuhakikisha hawashiriki
tukio au onyesho bila kuwa na mkataba na waandaaji kwani hali hiyo
inawafanya wadhulumiwe na kushindwa kudai haki zao kwa mujibu wa
makubaliano.
“Ni
lazima sasa wasanii wadai mikataba. Sisi tunawabana wakuzaji sanaa
(mapromota) kuambatanisha mikataba yao kabla hatujawapa kibali lakini
lazima na wasanii waoneshe wajibu wao kwa kudai mikataba na kutoshiriki
maonyesho bila makubaliano ya maandishi” alionya Shalua.
Alisisitiza
kuwa, Baraza litakuwa makini katika kufuatilia wadau wanaopewa vibali
vya kuendesha matamasha na matukio mbalimbali ya Sanaa na mara taratibu
na kanuni zitakapokiukwa halitasita kuchukua hatua za makusudi.
Na Alistides Kwizela
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)