BALOZI IDD SEIF ALITAKA JESHI LA POLISI KUIMARISHA ULINZI KATIKA FUKWE - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

BALOZI IDD SEIF ALITAKA JESHI LA POLISI KUIMARISHA ULINZI KATIKA FUKWE

Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi akitembelea nyumba za askari Polisi zilizojengwa huko Paje Mkoa wa Kusini Unguja ikiwa ni Shamra shamra za kutimia miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 
Na Yussuf Simai-Maelezo Zanzibar.
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi amelitaka jeshi la Polisi kuimarisha Ulinzi Zaidi katika sehemu za fukwe za Zanzibar ili kuondosha Uhalifu unaofanywa na watu wanaojifanya ni mapapasi wa Watalii. 
 
Makamo ameyasema hayo huko Paje mkoa wa kusini Unguja alipofungua Nyumba za Askari Polisi pamoja na kuweka jiwe la Msingi katika nyumba nyengine zinazoendelea kujengwa katika sehemu hio.
Balozi Seif amesema kuwa hivi sasa kuna vikundi mbalimbali vya watu wanaojifanya mapapasi wa Watalii na kupita katika Fukwe na kuwanyang’anya watalii ambao hukaa katika Fukwe na kujipumzisha.
 
Amezitaja fukwe za Nungwi, Bwejuu na Paje kuwa ndizo zinazopendelewa sana na wahalifu hao hivyo amelitaka jeshi hilo kuimarisha Ulinzi zaidi ili kuona wananchi pamoja na Watalii wanakuwa na utulivu na salama katika sehemu hizo.
 
Akizungumzia suala la Makaazi Balozi amesema,malengo ya Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar ni kuwapatia maisha bora na makaazi mazuri wananchi wake wote na hivyo itaendelea kujenga makaazi zaidi kila itakapokuwa na uwezo.
 
Nae Kamishna wa Polisi Zanzibar Mussa Ali Mussa ameahidi kuchukua hatua zaidi za usalama katika maeneo yaliotajwa na maeneo mengine ili kulinda maisha ya Raia pamoja na Mali zao.
 
Kadhalika amewataka wananchi wote kushirikiana na Jeshi la Polisi ili kuwafichuwa wale wote wanaojishughulisha na vitendo vibaya vya Unyang’anyi na Uporaji kwa Watalii na wananchi kwa jumla.
 
Ufunguzi wa Nyumba hizo za Polisi umekwenda sambamba na utowaji wa Vyeti kwa Wawekezaji wawili ambao ndio wadhamini wa Ujenzi huo,ambao ni Ivan Koden anaemiliki Hoteli ya Cystal Resort ya Paje na Hussen Alhashim anaemiliki Hoteli ya Grand Property ya Paje.(PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR).

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages