Picha
ya pamoja baina ya washindi wa bidhaa hiyo awamu ya kwanza pamoja na
washindi wa awamu ya pili, ambapo awamu ya kwanza washindi hao walipewa
zawadi za flash, Ipod, pamoja na t shirt kutoka katika benki hiyo.
Mshindi
wa kwanza Jackline Swai (kulia) akikabidhiwa zawadi ya Lap top na
Msadizi wa Meneja wa Azania Bank Tawi la Mbauda Hashim Ally Simchimbey.
Mshindi
wa Pili Ramadhani Mkorehe (kulia) akikabidhiwa zawadi ya Lap top na
Msaidizi wa Meneja wa Azania Bank Tawi la Mbauda Hashim Ally Simchimbey
Ulifika wakati wa msosi na hapa washindi wakiongozwa na Kirigiti Chacha Wamburawakijipakulia msosi.
Msosi ulianza kuliwa huku watu wakishusha moja moto moja baridi
Mshindi
wa Tatu Kirigiti Chacha Wambura akikabidhiwa hundi yenye thamani ya sh.
1.5 (kulia), akikabidhiwa hundi hiyo na Msaidizi wa Meneja wa benki
hiyo Hashim Ally Simchimbey.
Shindano hilo ni maalumu kwa wanafunzi ambao bank hiyo imeamua kutoa bidhaa inayoitwa ASPIRE ACCOUNT kwa lengo la kutoa morali ya kutumia huduma za kibenki kwa wanafunzi wa sekondari na vyuo.
Hafla hiyo fupi ilifanyika Januari 6,2012 kwenye hotel ya Golden Rose kwenye ukumbi wa Masaai hall, ambapo ilifuatiwa na tafrija fupi baadae.
Faida za wanafunzi kujiunga na bidhaa hizo ni kupata kadi ya mashine ( ATM) bure, hakuna makato ya mwezi, na kupata faida ya asilimia tano kila mwaka.
Pia bank hii imepunguza masharti kwa wanafunzi kufungua bidhaa hiyo ambapo hutoa vitambulisho vya shule pamoja na barua ya utambulisho kutoka kwa wakuu wa shule na inafunguliwa kwa zero balance ama kiwango cha kuanzia elfu kumi kwa mwanafunzi atakayemudu kutoa kiwango hicho.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)