Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba Atemebelea Maonyesho Ya Miaka 50 Ya Uhuru - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba Atemebelea Maonyesho Ya Miaka 50 Ya Uhuru

Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Afisa Masoko Mwandamizi wa Mfuko wa Akiba ya Wafanyakazi Serikalini (GEPF) James Mlowe (kushoto) juu ya majukumu ya mfuko huo na faida za kujiunga kwa wananchi. Waziri Mkuu huyo alipata maelezo hayo jana jijini Dar es salaam alipotembelea banda la Wizara ya Fedha wakati wa maonyesho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Mchambuzi wa Mifumo ya Kompyuta kutoka Idara ya Usimamizi wa Mifumo ya Fedha Wizara ya Fedha Elimu Sekeni (katikati) akitoa ufafanuzi kwa Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba (kulia) juu ya majukumu ya Idara hiyo . Waziri Mkuu huyo alipata maelezo hayo jana jijini Dar es salaam alipotembelea banda la Wizara ya Fedha wakati wa maonyesho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Maafisa wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu(NBAA) juu ya mafunzo mbalimbali yanayotolewa na Bodi katika kuimarisha taaluma ya ugavi na uhasibu nchini. Waziri Mkuu huyo alipata maelezo hayo jana jijini Dar es salaam alipotembelea banda la Wizara ya Fedha wakati wa maonyesho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Afisa Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Simoni Masawe(kulia) akitoa ufafanuzi kwa Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba (kushoto) juu ya jitihada mbalimbali zinazotumiwa na Mamlaka hiyo katika kuwaelimisha wafanyabiashara juu ya umuhimu wa kulipa kodi . Waziri Mkuu huyo alipata maelezo hayo jana jijini Dar es salaam alipotembelea banda la Wizara ya Fedha wakati wa maonyesho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba (kushoto) akiangalia machapisho mbalimbali ya Benki ya Uwekezaji Tanzania (TIB) yanayoonyesha fursa mbalimbali ambazo mwananchi anaweza kuzipata kupitia Benki hiyo katika kujikomboa kiuchumi. Waziri Mkuu huyo alipata maelezo hayo jana jijini Dar es salaam alipotembelea banda la Wizara ya Fedha wakati wa maonyesho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.Picha na Tiganya Vincent- MAELEZO--Dar es salaam

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages