
Rais
wa Zanzibar Dr Ali Mohd Shein akiangalia na kupata maelezo ya namana ya
kutengeneza gazeti katika chumba cha habari cha gaazeti la Zanziba Leo
wakati alipotembelea jengo hilo

Rais
wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr Ali Mohd Shein
akitoa maelezo kwa mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo zanzibar Yussuf
Omar Chunda wakati alipolitembelea jumba la zamani la kurushia
matangazo ya redio hapo rahaleo mjini zanzibar

Rais
wa Zanzibar Dr Ali Mohd Shein akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa
Idara ya Habari Maelezo zanzibar Yussuf Omar Chunda kulia ambae akitoa
maelezo ya jumba la zamani la kurushia matangazo ya redio hapo rahaleo
wakati Rais alipolitembelea jengo hilo.Picha na Yussuf
Simai-Maelezo-Zanzibar
----
Na Faki Mjaka Maelezo Zanzibar
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohammed Shein
amesema kuwa Jengo la Zamani la iliyokuwa Sauti ya Tanzania Zanzibar
lazima lirejeshwe katika hadhi yake ya zamani ili liweze kutumika katika
maswala mbalimbali ya Sanaa.
Amesema
kuwa Jengo hilo lina historia kubwa sana kwa upande wa Zanzibar na
Jengo ambalo ni madhubuti na lipo katika sehemu nzuri hivyo kurejeshwa
kufanya kazi kama zamani ya kuonesha michezo ya kuigiza na kutumika kwa
maonesho ya Vikundi vya Taarabu litarejesha hadhi na haiba katika
Zanzibar.
Dk.
Shein ameyasema hayo hivi leo wakati alipolitembelea Jengo hilo ili
kuona juu ya matumizi yake ya hivi sasa na hali lilivyo kutokana na
historia kubwa ya Jengo hilo kwa Zanzibar.
Amesema
kuwa Shirika la Gazeti la Serikali Zanzibar linalochapisha Gazeti la
Zanzibar Leo katika Jengo hilo litatafutiwa sehemu nyingine nzuri na
kubwa ili kuweza kufanya kazi zake kwa ufanisi zaidi na Jengo hilo
kuacha kutumika kwa ajili ya sanaa.
Akizungumzia
juu ya suala la iliyokuwa Sauti ya Tanzania Zanzibar amesema kuwa
imefika wakati kwa uongozi wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC)
kuandika historia ya kuanzishwa Redio hiyo ambayo ni ya mwanzo katika
Afrika Mashariki.
Dk.
Shein amesema kuwa si vizuri kwa Redio hiyo kuwa ya mwanzo kuanzishwa
wakati historia yake haionekani wala haipo hivyo ni wajibu viongozi wa
Shirika hilo kuchukua kila juhudi kuona kuwa wanaindaika historia ya
kuanzishwa kwa Redio hiyo pamoja na viongozi wake kuwekewa kumbukumbu za
picha wakiwemo watangazaji wake.
Aidha
Dk.shein ameutaka uongozi wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na
Michezo kulienzi na kulidumisha Jengo hilo kwa kulifanyia matengenezo
kwani amesema kuwa hivi sasa huwezi kupata jengo madhubuti na lenye
haiba yake hilo.
Akizungumzia
juu ya Habari Maelezo Zanzibar amesema kuwa hatua iliyochukuliwa ya
kuanza ujenzi wa sehemu ya Maktaba itasaidia sana katika uwekaji na
utunzaji wa kumbukumbu za matukio mbalimbali za Picha,Magazeti na
Majarida.
Mapema
Mkurugenzi wa Idara Habari Maelezo Zanzibar Yussuf Omar Chunda
alimuelezea Rais Shein historia ya Jengo hilo na matumizi yake ya hivi
sasa.

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)