Serengeti yadhamini pambano la Bunge SC Vs Baraza la Wawakilishi SC Ijumaa - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Serengeti yadhamini pambano la Bunge SC Vs Baraza la Wawakilishi SC Ijumaa

Katikati ni Mkurugenzi wa Mawasiliano kampuni ya SBL.Teddy Mapunda akikabidhi kombe kwa viongozi wa timu ya Bunge na Timu ya Baraza la Wawakilishi.Pichani kulia ni Kapteni wa timu ya Bunge,Mh Amos Makala na kushoto ni Mwenyeki wa timu ya Baraza la Wawakilishi,Mh Hamza Hassani Juma.
Mkurugenzi wa Mawasiliano kampuni ya SBL.Teddy,Mapunda (katikati), akizungumzia namna udhamini wao utakavyokuwa kwa timu hizo, wengine kulia na kushoto ni Nahodha wa timu ya Bunge, Mh Amos Makalla na Mwenyekiti wa timu ya Baraza la Wawakilishi, Mh Hamza Hassani Juma.
Viongozi wa Timu ya Wawakilishi nae akifafanua zaidi namna watakavyowakabili wapinzani wao Desemba 9 mwaka huu ndani ya Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Kapteni wa Timu ya Wabunge,Mh Amos Makala akizungumza ni namna gani wamejipanga kuhusiana na mechi hiyo itakayokuwa ya kusisimua dhidi ya mahasimu wao Timu ya Baraza la Wawakilishi kutoka Zanzibar.
Mkurugenzi wa Mawasiliano kampuni ya SBL.Teddy,Mapunda akizungumza mbele ya wanahabari mapema leo Makao Makuu ya ofisi hizo zilizopo Oysterbay,jijini Dar,kuhusiana na udhamini wa mechi kati ya Timu ya Wabunge na Timu ya Baraza la Wawakilishi kutoka Zanzibar,itakayofanyika 9 Desemba kwenye Uwanja wa Uhuru,ikiwa ni sehemu mojawapo ya kusherehekea miaka 50 ya Uhuru,aidha Teddy amesema kuwa udhamini wa timu hizo umegharimu kiasi cha zaidi ya milioni 65.
Mkurugenzi wa Mawasiliano kampuni ya SBL.Teddy Mapunda akikabidhi jezi kwa viongozi wa timu ya Baraza la Wawakilishi na kupokelewa na Mwenyeki wa timu ya Baraza la Wawakilishi,Mh Hamza Hassani Juma.
Mkurugenzi wa Mawasiliano kampuni ya SBL.Teddy Mapunda akikabidhi jezi kwa viongozi wa timu ya Bunge. Anaepokea Jezi hizo ni Kapteni wa timu ya Bunge,Mh Amos Makala na Kulia ni Mratibu wa Timu ya Bunge, Juma Nkamia.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages