Kampuni ya mawasiliano ya simu za
mkononi Vodacom Tanzania, imezindua huduma ya 'Young Africa Live'
itakayowawezesha wateja wake kupata taarifa sahihi za afya, mahusiano na
Mapenzi kuanzia leo Desemba Mosi mwaka huu.
Kupitia huduma hiyo ya kwanza nchini
wateja wa Vodacom watapata fursa ya kuunganishwa moja kwa moja na wadau
wa masuala ya afya na mahusiano ya jinsia ikiwa ni pamoja na kujibiwa
maswali watakayokuwa wakiuliza kupitia simu zao mkononi.
'Young Africa Live' ni huduma
inayowaunganisha wanajamii kihabari kupitia simu za mkononi na kutoa
burudani na fursa ya mazungumzo na kubadilishana taarifa
na uzoefu katika mada za mapenzi, ngono, mahusiano, jinsia na
afya ya uzazi
“Tunaimani kwamba huduma hii
itasaidia jamii hususan vijana ambapo kupitia taarifa za kiafya wataweza
kuwa na mahusiano yenye tija na kujikinga na maambuzkizi ya virusi vya
Ukimwi na Ukimwi”Alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Bw. Rene Meza
“Kila juhudi ni muhimu katika vita ya
kupunguza athari za virusi vya Ukimwi na Ukimwi, matatizo ya afya ya
uzazi katika jamii ikiwemo vifo. Taarifa sahihi ni nyenzo muhimu katika
mapambano haya, hivyo huduma hii ni wazi itapunguza pengo la ukosaji wa
habari muhimu za afya kwa wanajamii.”Ameongeza Rene.
Ili mteja wa Vodacom aweze kunufaika
na huduma hii ya kwanza nchini kutoka Vodacom anapaswa kuwa na huduma ya
Intaneti kwenye simu yake na kupitia Portal ya Young
Africa Live ataunganishwa na wanajamii wengine na wadau wa afya kwa
urahisi.
Gharama ndogo itatozwa kwa wateja wa
Vodacom wa malipo ya kabla. “Tunategemea vijana wengi kutumia
fursa hii kujifunza, kubadilishana mawazo na uzoefu juu ya masuala ya
afya na mahusiano na hatimae kuwa chachu ya mabadiliko ya tabia.”Alisema
Rene
Huduma ya 'Young
Africa Live' imefanya vizuri katika nchi ya Afrika Kusini na kuwa
tegemeo la chanzo cha habari kwa vijana ambao kupitia mazungumzo ya
pamoja yameweza kuwasaidia kubadili mitazamo yao katika mapenzi, 'Ngono'
na masuala ya afya ya uzazi.






No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)