Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza wakati alipokutana na
Watanzania waishio nchini Burundi jana usiku. Kushoto ni Balozi wa
Tanzania nchini Burundi, Dkt. James Mwasi Nzagi (kulia) ni Mwenyekiti wa
Kinamama wa Jumuiya ya Kinamama waishio Burundi, Siwajibu Hamis (wa
pili kulia) ni Mwenyekiti wa Vijana wa Jumuiya hiyo, Mutalemwa Julian.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiagana na baadhi ya Watanzania waishio Bujumbura Burundi, baada ya
kumaliza mazungumzo baina yao yaliyofanyika jana usiku na kujadili mambo
mbalimbali yanaoendelea katika Taifa la Tanzania.
Waziri wa Ulinzi na
Jeshi la Kujenga Taifa, Hussein Mwinyi (katikati) Naibu Waziri wa Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi J Mahadhi (kulia) Naibu
Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima, wakifurahia jambo kwa pamoja
wakati wakiwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bujumbura Burundi
wakisubiri kuondoka kurejea nchini leo baada ya kuhudhuria Mkutano wa
Nchi za Maziwa Makuu uliomalizika nchini humo juzi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Makamu wa Rais wa Burundi, Therence
Sinunguruza, wakati akiwa kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Burundi leo
mchana tayari kwa kuondoka nchini humo kurejea Tanzania baada ya
kumaliza shughuli za Mkutano wa Nchi za Maziwa Makuu, uliomalizika
Bunjumbura Burundi juzi.
Wasanii wa Kikundi
cha Ngoma ya asili cha Burundi wakionyesha umahiri wao wa kucheza ngoma
hiyo wakati wa hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa maalum kwa
ajili ya viongozi waliohudhuria Mkutano wa Nchi za Maziwa Makuu
Bujumbura Burundi. Hafla hiyo ilifanyika juzi jioni baada ya kufungwa
rasmi kwa mkutano huo.

Mtoto akionyesha
umahiri wake wa kucheza miondoko ya ngoma hiyo wakati wa hafla ya
chakula cha jioni.
Askari wakiimalisha
ulinzi kwenye Uwanja wa Ndege wa Bujumbura.











No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)