Meneja
Mauzo wa Kampuni ya Vodacom Kanda ya Kaskazini Bw. Jerome Munishi
akimkabidhi Mkurugenzi wa kituo cha watoto yatima cha Matonyak Bi. Emmy
Ndeumo cha Mjini Arusha zawadi mbalimbali kwa ajili ya kuwawezesha
watoto kusherehekea vema siku kuu ya Krismasi. Misaada hiyo
iliyojumuisha vykula na vifaa vya shule ilikabidhiwa jana ikiwa ni
sehemu ya kampeni ya Vodacom Share and Care.
kazi wa Vodacom kanda ya kaskazini Rehema Ndunguru akigawa viburudisho watoto wa kituo cha Matonyak cha mjini Arusha ikiwa ni sehemu zawadi mbalimbali za krismas zilizotolewa kituoni hapo kupitia kampeni
ya Vodacom Share & Care inayoendeshwa kila ifikapo Disemba.
Vodacom imekabidhi misaada mbalimbali kwa vituo sita vya watoto yatima
na wanaoishi katika mazingira magumu vya mjini Arusha jana.
Meneja
Mauzo wa Kampuni ya Vodacom Kanda ya Kaskazini Bw. Jerome Munishi
akimkabidhi Mkurugenzi wa kituo cha watoto yatima cha Matonyak Bi. Emmy
Ndeumo cha Mjini Arusha zawadi mbalimbali kwa ajili ya kuwawezesha
watoto kusherehekea vema siku kuu ya Krismasi. Misaada hiyo
iliyojumuisha vykula na vifaa vya shule ilikabidhiwa jana ikiwa ni
sehemu ya kampeni ya Vodacom Share and Care.
Wafanyakazi
wa kampuni ya Vodacom Kanda ya kaskazini wakiwa katika picha ya pamoja
ya kumbukumbu na watoto pamoja na viongozi wa kituo cha yatima cha
Matonyak cha mjini Arusha. Wafanyakazi hao walifika kituoni hapo jana
kukabidhi zawadi mbalimbali za krismasi ikiwa ni sehemu ya kampeni ya
Vodacom Share & Care ambapo jumla ya vituo sita vya yatima vya mjini
Arusha vilipatiwa misaada.

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)