Afisa
Habari wa UN Information Centre (UNIC) Usia Nkhoma Ledama
akiwakaribisha wageni waalikwa katika semina ya mafunzo kwa vijana juu
ya matumizi ya mtandao katika kuhamasisha haki za Binadamu iliyofanyika
katika Ofisi za UN Information Centre.
Mtaalamu
wa IT na Mwanaharakati wa Haki za Binadamu kutoka Kamisheni ya Haki za
Binadamu na Utawala Bora (CHRAGG) Bw.Wilfred Warioba akielezea jinsi
mitandao ya Kisasa ya Mawasiliano kama vile Facebook, Twitter na Blogs
zinavyofanyakazi na zinavyoweza kutumika kupashana Habari na
Kuelimishana ambapo pia amesema iwapo itatumika vibaya inaweza kuelta
madhara makubwa kwa watumiaji. Katikati ni Mzungumzaji Mkuu Mwalikwa
kutoka CHRAGG Bw. Ayoub Rioba na Afisa Habari wa United Nation
Information Centre Bi. Stella Vuzo.
Mzungumzaji
Mkuu Mwalikwa kutoka CHRAGG Bw. Ayoub Rioba akielezea nafasi ya vijana
kama wahusika wakuu katika matumizi ya Mitandao hiyo ambapo amewataka
vijana kuwa watetezi wa haki za Binadamu kwa kutoa taarifa pale
wanapoona haki hizo zinakiukwa.
Wanafunzi na wageni waalikwa waliohudhuria mafunzo hayo wakitazama filamu "White and Blacks: Crimes of Color" inayozungumzia Maisha, Haki na Adha wanazokabiliana nazo jamii ya watu wenye Ulemavu wa ngozi (Albino).
Afisa
Habari wa Temeke Youth Development Network (TEYODEN) Humphrey Shao
akifafanua jambo kuhusiana na matumiz ya mitandao kama njia ya
mawasiliano
Wanafunzi na wageni waalikwa waliohudhuria mafunzo hayo wakitazama filamu "White and Blacks: Crimes of Color" inayozungumzia Maisha, Haki na Adha wanazokabiliana nazo jamii ya watu wenye Ulemavu wa ngozi (Albino).
Afisa
Habari wa United Nationa Information Centre Usia Nkhoma akigawa nakala
za Filamu ya "White and Black: Crimes of Color". kwa wanafunzi
wawakilishi wa shule zilizohudhuria mafunzo hayo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)