RAIS DK. JAKAYA KIKWETE AONGOZA WATANZANIA KATIKA SHEREHE ZA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

RAIS DK. JAKAYA KIKWETE AONGOZA WATANZANIA KATIKA SHEREHE ZA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA

Rais Dk. Jakaya Kikwete akipungia mkono wananchi wakati alipowasili kwenye uwanja wa uhuru kwa ajili ya kuongoza sherehe za miaka 50 ya Tanzania.

Rais jakaya Kikwete akipokea heshima wakati mizinga ikipigwa na jeshi la wananchi kwa heshima ya Rais.
Hiki ni kikosi cha Jeshi la wananchi wanamaji kikiwa tayari kutoa heshima kwa amiri jeshi mkuu na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tamnzania Dk. Jakaya Kikwete.
Rais Jakaya Kikwete akikagua vikosi vya ulinzi na usalama wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania kikosi hiki ni cha Jeshi la Wananchi wanaume.
Rais Jakaya Kikwete akielekea Jukwaa kuu mara baada ya kukagua gwaride katika sherehe za miaka 50 ya uhuru wa Tanzania kwenye uwanja wa Uhuru huku akiwa ameongoza na na Mkuu wa Majeshi nchini Jenerari Davis Mwamunyange.
Rais Jakaya Kikwete akikagua vikosi vya ulinzi na usalama wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania kikosi hiki ni cha Jeshi la Wananchi wanawake
Rais Dk. Jakaya Kikwete akisalimiana na viongozi wa nchi mbalimbali waliohudhuria katika maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania yanayofanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam mchana huu hapa akisalimiana na Rais wa Namibia Mhshimiwa Hifikepunye Pohamba. FULLSHANGWE inakumuvuzishia moja kwa moja matukio ya maadhimisho hayo kutoka kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam ili kukujuza mambo mbalimbali yaliyojiri katika sherehe hizo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages