UMATI WA WATU WAJITOKEZA UWANJA WA UHURU KUSHUHUDIA SHEREHE ZA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

UMATI WA WATU WAJITOKEZA UWANJA WA UHURU KUSHUHUDIA SHEREHE ZA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA

Mabalozi mbalimbali wakishuka katika basi maalum la Wizara ya Mambo ya Nje mara baada ya kuwasili katika sherehe za Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania ,zinazofanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam zikihudhuriwa na wageni mbalimbai, mabalozi wakuu wa nchi kadhaa za Afrika, Asia na Ulaya na viongozi wa Serikali wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk Jakaya Kikwete. Fullshangwe iko katika eneo la tukio ikikumuvuzishia matukio mbalimbali yanayojiri katika sherehe hizo.
Waheshimiwa wabunge na makatibu wakuu wa Wizara mbalimbali wakiteremka kwenye mabasi yaliyowabeba kwa ajili ya kushiriki katika sherehe za miaka 50 ya uhuru wa Tanzania
Mambo yameiva katika sherehe za miaka 50 ya uhuru wa Tanzania kama unavyoona kundi la bendi ya Msondo ngoma likiwatumbuiza wageni waalikwa mbalimbali katika sherehe hizo
Watu mbalimbali wakiwa wamefurika katika uwanja wa Uhuru.
Vijana wa halaiki wakiwa katika staili maalum ya ukaaji katika sherehe hizo.
Mwanamuziki mpiga gitaa la Solo wa bendi ya Msondo akipiga gitaa lake katika sherehe hizo wakati bendi hiyo ikitoa burudani.Picha Na John Bukuku Wa Full Shangwe Blogu

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages