Na Mwandishi Wetu, jijini Dar
BENDI ya muziki wa dansi ya
African Stars “Twanga Pepeta International imewasili jana kutoka,
London, Uingereza na kuweka mikakati yake ya kuhimarisha soko la
kimataifa na la hapa nyumbani.
Kauli hiyo ilitolewa na kiongozi wa bendi hiyo, Luizer Mbutu alipokuwa anazungumzia mafanikio na changamoto za maonyesho yao yaliyofanyika nchini Uingereza.
Luizer alisema kuwa wamepata mafanikio makubwa katika maonyesho hayo ya wiki mbili huku moja likiwa la kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania.
Alisema kuwa tofauti na ziara yao
ya kwanza ya mwaka 2005, safari hii walikwenda kufanya shoo huku
wakizinadi CD na DVD za albamu zao za nyuma zikiwa katika maonyesho ya
‘live’ nay a kawaida ambazo walifanikiwa kuziuza zote.
“Kwa
kweli tumefarijika sana na maonyesho na kufanikiwa kuuza kazi zetu
nchini Uingereza, kazi iliyobakia sasa ni kuhimarisha soko hilo huku
tukifanya kazi kama hiyo hiyo hapa nyumbani,” alisema Luizer.
Alisema kuwa maonyesho yao yalijaza watu mbali mbali wa mataifa tofauti na kupata mwaliko mwingine ambao uongozi utaamua lini watarejea huko.
“Napongeza uongozi wa ASET chini ya Mwenyekiti, Msiilwa Baraka na Mkurugenzi, Asha Baraka kwa kufanikisha ziara
hii ya tatu kwa bendi kufanya maonyesho Ulaya, mwaka 2005 tuliweza
kufanya maonyesho katika nchi tano za Scandinavia na mwaka uliofuata
tukaingia London kwa mara ya kwanza,” alisema.
Alisema kuwa hawakuwa wanakaa
tu kusubiri kazi za kufanya maonyesho kwani wameweza kutunga nyimbo
mbili, mmoja unajulikana kwa jina la Back to London uliotungwa na Chalz
Baba na Uzuri wa Mwanamke mke siyo Tabia bali ulivyopendezewa uliotungwa
na Saleh Kupaza.
Alisema kuwa nyimbo hizo zitafanyiwa mazoezi ili kuzihimarisha na kuanza kupigwa katika maonyesho yao mbali mbali ya mwisho wa wiki hii.
Mkurugenzi
wa bendi hiyo, Asha Baraka aliwapongeza wote waliofanikisha ziara hiyo
na kusema kwa ssa wanajipanga kwa ajili ya maonyesho ya hapa nyumbani na ziara nyingine za nje ya nchi.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)