
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),Eugen
Mikongoti (katikati) akionyesha Tuzo ya Utoaji wa Huduma Bora za
kijamii baada ya kuibuka na ushindi wa jumla katika mashindano ya
Mashirika ya Hifadhi za Jamii kwa nchi za Ukanda wa Afrika,baada ya
kukabidhiwa na Rais wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Kimataifa (ISSA)
,Bw. Errol Frank Stoove (kushoto) kwenye hafla fupi iliyofanyika katika
hoteli ya Mount Meru jijini Arusha usiku wa kuamkia leo.Kulia ni Muweka
Hazina wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Kimataifa (ISSA),Philippe Conus.

Rais
wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Kimataifa (ISSA) ,Bw. Errol Frank
Stoove (kushoto) akikabidhi tuzo mbili za Utoaji wa Huduma Bora za
Kijamii kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Mashirika ya Umma
(PPF) William Erio (katikati) katika hafla fupi ya utoaji tuzo hizo
iliyofanyika usiku wa kuamkia leo katika hoteli ya Mount Meru,jijini
Arusha.

Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Akiba kwa Wafanyakazi Serikali (GEPF), Daudi Msangi
akipokea tuzo ya Utendaji Bora Afrika kutoka kwa Rais wa Mfuko wa
Hifadhi ya Jamii wa Kimataifa (ISSA) ,Bw. Errol Frank Stoove (kushoto)
baada kushinda katika mashindano yaliyozishirikisha nchi 19 katika
Ukanda wa Afrika. Kulia ni Mweka Hazina wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa
Kimataifa (ISSA),Philippe Conus.

Rais
wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Kimataifa (ISSA) ,Bw. Errol Frank
Stoove (kushoto) akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa
Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),Eugen Mikongoti (pili kulia) ambaye Mfuko
wake ndio Ulioshinda Tuzo ya jumla Utoaji wa Huduma Bora za Kijamii kwa
Mashirika ya Hifadhi za Jamii kwa nchi za Ukanda wa Afrika,akifuatiwa na
Katibu Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Kimataifa (ISSA),Bw.
Hans-Horst Konkolewsky Pamoja na Mweka Hazina wa Mfuko wa Hifadhi ya
Jamii wa Kimataifa (ISSA),Philippe Conus.

Washindi wa Tuzo za Utoaji wa Huduma Bora za Kijamii wakiwa pamoja na Wadau waliowasindikiza kwenye hafla hiyo.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)