*WAPIGWA PA, WAPO CHINI YA ULINZI ARUSHA KESHO KUSAFIRISHWA KWENDA CONGO.
MWANAMUZIKI
mahiri wa miondoko ya dansi aliyepata kujizolea sika kem kem nchini
wakati akiwa na bendi ya FM miaka ya nyuma kabla ya kujiengua na kuunda
kundi lake lililojulikana kwa jina la Stono Musica, Ndanda Cosovo
‘Kichaa’ amekamatwa masaa machache jijini Arusha pamoja na wanamuziki wa
bendi yake mpya.
MWANAMUZIKI
mahiri wa miondoko ya dansi aliyepata kujizolea sika kem kem nchini
wakati akiwa na bendi ya FM miaka ya nyuma kabla ya kujiengua na kuunda
kundi lake lililojulikana kwa jina la Stono Musica, Ndanda Cosovo
‘Kichaa’ amekamatwa masaa machache jijini Arusha pamoja na wanamuziki wa
bendi yake mpya.
Akizungumza
na Mtandao wa Sufianimafoto kwa njia ya simu, Ndanda Cosovo, alisema
kuwa amekamatwa yeye pamoja na wanamuziki wake wote na kuwekwa chini ya
ulinzi ambapo kwa sasa wanasubiri kupelekwa Rumande hadi kesho
watakaposafirishwa kurudi kwao Kongo.
Aidha
Ndada alisema kuwa ameshangazwa na uongozi wa Uhamiaji kukagua vibali
vyake vya kuishi nchini na kumwambia kuwa vibali hivyo ni ‘Feki’ hali ya
kuwa alikata na kulipia vibali hivyo jijini Dar es Salaam.
“Mimi
nashangaa sana kama Mkurugenzi wa Uhamiaji anaweza kupokea pesa na
kisha akatoa vibari Feki, hii si sawa kwani mimi nilikuwa nikiishi
Tanzania kwa uhalali na kufuata taratibu zote na ndiyo maana nikawa
nikifanya kazi zangu bila kificho, leo nakamatwa nakuambiwa vibari
vyangu ni feki kwa kweli nimesikitika sana,
Napenda
kuwaageni marafiki zangu wote mbaki salama kwani tuliishi kwa amani na
kusaidiana kama ndugu leo hii naambiwa nimevunja sheria mbona
hawajaniambia hivyo tangu nilipokuwa nikiwalipa pesa za vibari??”
alimaliza kwa kuhoji Cosovo.Habari Kwa HIsani Ya Sufiani MAfoto








No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)