TASWIRA ZA UFUNGUZI WA JENGO LA PSPF NA RAISI KIKWETE HAPO JANA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

TASWIRA ZA UFUNGUZI WA JENGO LA PSPF NA RAISI KIKWETE HAPO JANA

Rais Dk. Jakaya Kikwete akihutubia wageni waalikwa wakati alipozindua jengo jipya la kitega uchumi la Golden Jubilee Towers, linalomilikiwa na Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) lililopo barabara ya Ohio jijini Dar es salaam. Jengo hilo limegharimu zaidi ya shilingi bilioni 60 na lina minara miwili mmoja ukiwa na ghorofa 22 na mwingine ukiwa na ghorofa 13 na litakuwa na ofisi, maduka pamoja na mgahawa unaozunguka, ambapo ukienda katika mgahawa huo utaweza kuona pande zote za jiji la Dar es salaam, lakini pia jengo hilo lina eneo la kuegesha magari yapatayo 300 kwa wakati mmoja.
Rais Dk Jakaya Kikwete akifunua pazia kuashiria uzinduzi rasmi wa jengo hilo uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
Rais Dk.Jakaya Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi jengo la Golden Jubilee Towers jijini Dar es salaam leo, kulia ni George Yambesi Mwenyekitiwa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika hilo na kushoto ni Mustafa Mkulo Waziri wa Fedha na Uchumi. 
Hili ndiyo jengo lenyewe la Golden Jubilee Towers lilivyo.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nao wamehudhuria katika uzinduzi huo ili kujionea mambo yalivyokuwa na kuwamuvuzishia wananchi.Picha Na John Bukuku Wa Full Shangwe Blogu

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages