Mkurugenzi
Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza (kushoto) akifafanua jambo kwa
waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa huduma ya pamoja na kampuni ya
Western Union, uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania waliohudhuria katika uzinduzi wa
huduma ya M pesa itakayokuwa inatolewa kwa pamoja na kampuni ya Western
Union.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza (kushoto) akishikana mkono na
Mkurugenzi Mtendaji wa Western Union wa Afrika Mashariki na kusini,
Karen Jordaan,ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa huduma ya pamoja na kampuni
ya Western Union ambapo wateja wa simu za mkononi wa Vodacom nchini
watakuwa wakipokea pesa kutoka nje ya nchi moja kwa moja kwa kutumia
huduma ya Vodacom M-PESA.
*******************************************
*Wateja wa Vodacom M-PESA sasa kupokea pesa kutoka nje ya nchi kupitia huduma ya Western Union
Na Mwandishi Wetu, Jijini Dar
Kampuni
ya Western Union na Vodacom Tanzania zimezindua huduma mpya ambapo
kuanzia sasa wateja wa Vodacom Tanzania watapata pesa zao kupitia huduma
ya M-PESA.
Kwa
mara ya kwanza wateja wa simu za mkononi wa Vodacom nchini wanao uwezo
wa kupokea pesa kutoka nje ya nchi moja kwa moja kupitia huduma ya
Vodacom M-PESA.
Huduma
ya Mobile Wallet ambayo ndio itakaoyotumika kuwaunganisha wateja wa
Western Union na M-PESA ni ya haraka, kuaminika na uhakika kwa marafiki
na wanafamilia kutuma fedha kutoka nje ya nchi. Mtumaji anachopaswa
kufanya ni kufika kwa mmoja kati ya mawakala 108,000 wa Wetsern Union katika nchi zaidi ya 65 ulimwenguni kote na kutuma pesa hizo ambazo zitatumwa moja kwa moja kwenda kwenye akaunti ya mpokeaji ambaye ni mteja wa Vodacom M-PESA.
Mpokeaji
wa fedha hizo atatumiwa ujumbe wa kumjulisha kuingia kwa pesa hizo
katika akunti yake ya M-PESA na kwamba ataweza kuzitoa pesa hizo kupitia
moja ya wakala zaidi ya 15000 wa M-PESA kupitia taratibu za kawaida za
utoaji pesa.
“Siku
zote Vodacom hutafuta suluhisho la mahitaji ya wateja wake kupitia
huduma bunifu kama hii ambayo tunaizindua leo”Alisema Mkurugenzi
Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bw. Rene Meza. Matumizi ya M-PESA
yanaongezeka mwezi hadi mwezi na kumekuwepo kilio kutoka kwa wateja wetu
wakitaka huduma hiyo kuvuka mipaka ya nchi, kilio ambacho tunafuraha
kuona leo tumekipatia suluhisho kutoka M-PESA pekee.
Kuanzia
leo wateja wa M-PESA wanaweza kupokea pesa kutoka kwa ndugu na jamaa
wanaoishi nje ya nchi ikiwemo Kenya na Uganda “Hakuna gharama zozote za
ziada katika kuchukua pesa hizo kutoka kwa wakala zaidi ya gharama za
kawaida za utoaji wa pesa.”Aliongeza Rene
Vodacom
M-PESA ilizinduliwa mwaka 2008 na sasa ina wateja zaidi ya milioni tisa
ikifanya miamala zaidi ya milioni moja kwa siku na ni huduma ambayo ni
chagua la kwanza kwa wananchi katika kutuma na kupokea pesa pamoja na
kufanya malipo mbalimbali ikiwemo huduma za maji na umeme, kuongeza
salio, kulipa kodi, kununua tiketi za ndege n.k.
Western
Union inaendelea kutoa huduma bora ikiwa kampuni inayoongoza katika
huduma za utumaji wa pesa kutumia miundombinu yake iliyoenea ulimwenguni
kote ikiwa na vituo zaidi ya 108000 katika nchi 65 na mikataba ya
kibiashara na makampuni ya simu zaidi ya kumi duniani.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)