Katika pita pita zangu hii leo nikiwa anga za kamachumu km 2 kabla ya
kuingia mjini Milama,Nalazimika kufika kwenye nyumba ya mushonge nipati
walau picha na uhalisia wa ndani.
Nyumba ipo katikati ya shamba zuri la migomba yenye afya!!!
Ikiwa
kwenye mazingira safi imewekewa uzio wa matete(embingo kama wasemavyo
wao)nakumbuka enzi hizo matete yakitengeneza vitanda vya kulalia binafsi
nimepitia maisha hayo.
Baadhi ya viunga vya Kamachumu hii leo.
Yaap
moja kwa moja nakanyaga kwenye mji wa Kamachumu,Mji wenye hekaheka
nyingi,wadau wengi ni watata sana,Mji huu ndiyo chimbuko la maaskofu
wakubwa na maarufu tukianza na Askofi Kibila na hapo hapo anazaliwa
Cardinal wa kwanza wa Afrika Cardinal Laurean Rugambwa
Watu maarufu walitokea hapo akina Anthony Rugangila,Kalinjuma,na Ntonini,Haji Hamad,Byabusha,Mzee Songoro aka Karasha,familia ya Bukenya alikadhalika Zakalia Mugyabuso Petro Nshange aka (kibunda) na Christopha Ngaiza wote ni marehemu
Majemedali wengi kama bora Imani,Haji Birundulu na Haji Kabalala,Mzee Kabea na Haji Hamad nitakua sijatenda haki nisipo mkumbuka Bandeko na familia nzima ya akina Fresh.
Pia ipo familia ya al-squar ndio akina mawingu ,Adara na wadau wengine wengi hii ni kwa mkutasari tu!!!
Kwa sasa wapo akina Hamed Kiwanuka ,Haji Jaffary, Veda Rugabela,Mdau Myaga , Mzee Thadeo Iluganyuma na Mdau Sued ukanda wa Rutabo akiwepo Mzee Nestory Kato, mdau Chamisili na mwalimu Mastura.Picha Na Mdau Mc Baraka Wa Bukoba Wadau
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)